Una post picha Una Dripu hospital mitandaoni?

Yales

JF-Expert Member
Joined
Oct 3, 2015
Posts
517
Reaction score
528
Wakuu kuna watu akili zao zinawatosha wenyewe tu, Yani kuna ndugu yangu hapa kapost picha yuko na madripu Hospital Facebook huku akiomba Aombewe huu ni ulimbukeni au? Kuna Wa mama wa makamo tu wanahangaika kweli na social network kutwa kuchwa kupost picha marq wako bar mara wako vyumbani kwao yani wana ji exposure too much,

Binafsi situmii jina lolote halisi mitandaoni wala sijawah kuweka picha zangu mitandaoni waziwazi

Najua ni maisha yao na wala hayanihusu ila tu Naruhusu POVU kwa wale wakomoromije na wenye haka kaulimbukeni
 
Weka picha yake

Mtanisamehee wenye nafasi hii
 
Ingawaje huwezi kumpangia Mtu yeyote namna ya kuishi ila hilo nalo ni moja ya matokeo hasi ya Mapokezi ya Utandawazi..,
 
Wanatafuta kiki labda
 
Hao bana wanadhan mitandao ni kila kitu. Mie nshawafungulia thread maalumu kwa ajili yao. Kuna mmoja yupo msiban akaweka picha wamebeba jeneza akaandika yupo msiban anakula bata

Aisee facebook kuna vituko
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…