Unaamini nini?

Kigundu

Member
Joined
Jul 28, 2015
Posts
79
Reaction score
24
Wengi wa wanadamu wamechanganyikiwa, hawajui wawe na msimamo wa imani juu ya nguvu gani kiroho. Wengi wameishia kuwa vuguvugu, si moto wala si baridi!

Kwa mganga wa kienyeji wanaenda na kinga za maisha yao wanapata huko, si rahisi kumkuta mtu hasa Afrika hana alama hasa chale kwenye mwili wake ambazo huaminiwa kuwa kinga dhidi ya mashambulizi ya kishirikina au kichawi hii huambatana pia na uwekaji wa mizizi au hirizi kwenye miji yao na wakati huo huo huingia makanisani kwenye ibada kumwabudu MUNGU MWENYEZI, huko hujifanya wako safi na wanamtumainia na kumtegemea BWANA YESU KRISTO kuwa mwokozi na kinga ya maisha yao.

Huu ni upuuzi inatakiwa uwe na imani yenye msimamo wa MUNGU mmoja usimchanganye na ushetani wa namna yoyote ile, madhara ya kuchanganya ni kukosa msaada pale shetani anapokuhitaji wewe au mwanao kuzimu(kukuua), kwani mwivi(shetani) haji ila kwa kuiba, kuua na kuharibu hatma yake ni kukufikisha jehanamu.

TUBU LEO, MTEGEMEE MUNGU WA MAJESHI YEYE ATOSHA KWA 100%, usiiabudu mizimu(miungu).
 
Shetani ni nani?

Shetani ni baba wa uongo, ni muasi, ni mharibifu na ni mungu wa watenda dhambi wote na waabudu miungu. Makazi yake kwa sasa ni kuzimu anasubiri muda ufike atupwe jehanamu, MKATAE USIMFUATE, MTAFUTE MUNGU WA HAKI, MTAKATIFU, MWEZA WA YOTE, BWANA WA MAJESHI, MUUMBAJI, MUNGU WA miungu, KWA YESU KRISTO HAKIKA UTAOKOKA.
 

Kumbe? Sasa ndugu yangu naomba unifungue na mimi nimjue MUNGU WA HAKI, MTAKATIFU, MWEZA WA YOTE, BWANA WA MAJESHI, MUUMBAJI, MUNGU WA miungu.
Huyu shetani kutoka wapi ndugu Kigundu
 
Last edited by a moderator:
umesema kweli,vuguvugu wako wengi sana. i think Manipulation ndio tatizo linalopelekea haya yote..
 
Kumbe? Sasa ndugu yangu naomba unifungue na mimi nimjue MUNGU WA HAKI, MTAKATIFU, MWEZA WA YOTE, BWANA WA MAJESHI, MUUMBAJI, MUNGU WA miungu.
Huyu shetani kutoka wapi ndugu Kigundu

Shetani awali alikuwa malaika mkuu huko mbinguni, lkn kutokana na kujawa na tamaa za kujiinua zaidi kuliko BWANA MUNGU akaanzisha(akaasi) vita dhidi ya utawala uliotukuka na mtakatifu wa MUNGU matokeo yake alishindwa vibaya sana na kutupwa chini na nafasi yake haikuonekana tena mbinguni(soma biblia takatifu siwezi kukupa mistari ya kusoma kwani itakufanya uwe mvivu wa kusoma bible), baada ya kutupwa duniani kazi yake sasa ni kuharibu kazi ya mikono ya MUNGU kwa mfano hufanya kila linalowezekana kumharibu mwanadamu kwa kumfanya atende dhambi. Hakika ukiwa mtende dhambi tambua shetani kakuharibu, TUBU ILI DAMU YA YESU KRISTO IKUFANYIE MATENGENEZO KISHA ACHA KABISA DHAMBI.
 
Last edited by a moderator:
nauliza, shetani hakamatiki akafungwa ili tuwe huu nae, maana anatusumbua sisi watu wa mungu
 
nauliza, shetani hakamatiki akafungwa ili tuwe huu nae, maana anatusumbua sisi watu wa mungu

Hahahaha acha masihara ina maana wewe hutaki kupambana na Shetwaini na maovu yake bali akamatwe tu ili sie wana wa Mungu tuwe freeeeeee
 
nauliza, shetani hakamatiki akafungwa ili tuwe huu nae, maana anatusumbua sisi watu wa mungu

Shetani hana ujanja wa kumsumbua mwana wa MUNGU ambaye roho mtakatifu anakaa ndani yake kweli kweli, hatma ya mambo yote ni pale shetani, mapepo, majini na wanadamu waliomuasi MUNGU(watenda dhambi) watakapotupwa ktk ziwa la moto(jehanamu) siku ya mwisho na watakatifu wote watakapoirithi mbingu mpya na nchi mpya na kuishi maisha ya furaha na amani milele yote. Haleluya sifa na utukufu ni vyake BWANA MUNGU, ahadi zake zadumu milele na hazibadiliki kamwe. Ndugu yangu MUNGU hajipingi mwenyewe kilichokwisha pangwa kimepangwa hakitabadilika, hatma ya shetani ilishapangwa.
 

Samahani ndugu yangu sikuona notification.
Asante kwa kunijibu lakini kwa majibu wa biblia Mungu ni muumbaji wa kila kitu, ana upendo mkuu/anavipenda viumbe vyake vyote, yeye hujua mwanzo kabla ya mwisho na mwisho kabla ya mwanzo. Kwa maana kwamba kabla hajakiumba kiumbe chochote kilichoumbika yeye hutazama mwanzo wake kwanza mpaka mwisho na hurudi tena kutazama mwisho wake mpaka mwanzo na ndipo hukiruhusu kiwepo/umbika.
Sasa swali langu ni hili. Huyu shetani kabla ya kuumbwa kwake maisha yake yalijulikana yote, yaani Mungu alijua tarehe fulani ataasi/ataanzisha vita dhidi ya utawala wake lakini akamuumba tu. Sasa huyu shetani atakuwa na dhambi gani wakati muumba wake aliyajua maisha yake yote hata kabla ya kuumbwa kwake?? Kumbuka Mungu ni mkamilifu sana na ni mtakatifu sana, ni mwenye upendo kuliko binadamu.
Kwanini Mungu mwenye ufahamu mkubwa kuliko sisi hakuyatilia maanani matokeo mabaya ambayo aliyasababisha/ameyasababisha huyu shetani wakati sisi tumeyaona hayo?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…