Mwamba1961
JF-Expert Member
- Dec 10, 2016
- 626
- 409
Habari zenu,
Aisee ni vitu gani muhimu vya kuangalia wakati nachukua gari jipya au lililotumika?
Aisee ni vitu gani muhimu vya kuangalia wakati nachukua gari jipya au lililotumika?
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Unaponunua gari kuna mambo mengi ya kuangalia....Habari zenu,
Aisee ni vitu gani muhimu vya kuangalia wakati nachukua gari jipya au lililotumika?
gari jipya ni hmgharama kubwa sana na ndiyo maana ni watu wachache sana kwenye nchi yetu wanamudu kununua gari jipya
Hapa umetoa darasa zuri sana washindwe wao.Unaponunua gari kuna mambo mengi ya kuangalia....
Uchumi wako, Matumizi yako na Ukubwa wa injini.(cc)....yaani unatakiwa ununue gari ambalo utalimudu mafuta na huduma nyinginezo.
1 .Gari jipya..
Gari jipya hapa tunazungumzia gari ambalo ni 0 km....yaani limetoka kiwandani ukalinunua na wewe ndiyo unakuwa mtumiaji wa kwanza.
Unaponunua gari jipya suala la msingi la kuangalia ni je, unanunua gari hilo kwa matumizi yapi? Biashara?Familia? Au kubeba mizigo? na kadhalika
Lakini pia unaponunua gari jipya unaangalia uchumi wako kwa sababu gari jipya ni hmgharama kubwa sana na ndiyo maana ni watu wachache sana kwenye nchi yetu wanamudu kununua gari jipya.
2. Gari la Mtumba kutoka JAPAN, SINGAPORE, ULAYA au AMERICA.
Magari ya mtumba ndiyo magari yanayoongoza kwa kununuliwa sana hapa nchini kulingana na bei zake kuwa chini.
Mara nyingi watanzania tumezoea mtumba kutoka Japan huko Beforward.......watu wengi wamekuwa wakijidanganya kuwa wameagiza gari jipya kutoka Japan ilihali ADOmeter inasoma mfano km 10,000.
Hili Siyo gari jipya bali ni gari linaloletwa kwenye Mazingira mapya..
Unaponunua mtumba kutoka Japan,Ulaya, Singapore au Marekani....kumbuka hawa wenzetu ni watunzaji na wanazingatia kanuni zote za utunzaji wa gari, hivyo hii hufanya kuwa na uhakika kwa asilimia kubwa kubwa mtumba wa gari unaotaka kuagiza hauna shida sana....
Unaponunua mtumba wa gari suala la msingi la kuzingatia ni Matumizi yako (Je unahitaji gari la matumizi gani.), Ushuru wa TRA ili usije ukaliacha bandarini, Muundo wa gari unaokupendeza, Aina ya gari mf Toyoga, Nissan, Suzuki, Audi,BMW nk., lakini pia unaangalia mazingira utakayokuja kutumia gari lako. Je, utakuwa unaliendesha mjini tu au na huko mashambani na milimani..
Jambo jingine la unaponunua gari la mtumba ni kuangalia Umri wa gari toka lilipotengenezwa japo kuna watu wanapenda magari ya zamani, pia kama unanunua mtumba wa gari angalia gari lenye ADOmeter inyosoma chini ya Km 100,000....japo suala la mile age halina guarantee kwamba gari ni zima.
Kuna mabo mengine unayoweza kuyaangalia kwenye picha za gari husika mfano kama limebondeka mahali watakuwekea picha.
Baada ya kuangalia mambo hayo, unatafuta kampuni unayodhani itakidhi haja yako, kisha unaagiza kupitia wao au wakala wao mfano Beforward, SBT na wengineo wengi..
Mtumba ambao hujatumika bongo, pia unaweza kuupata hapa hapa nyumbani kwenye Yard za kuuza magari..
3. .Gari la mtumba lililotumika nje ya nchi, kisha likatumika hapa Tanzania.
Hili ni gari lilionunuliwa nje ya nchi likiwa mtumba, mbongo kalitumia kisha naye kaamua kuliuza kwa sababu moja au nyingine....
Pengine analiuza ili aongezee pesa anunue lingine, Pengine analiuza alipe mkopo wa benki au ada za watoto au PENGINE ANALIUZA KWA SABABU LINAMSUMBUA NA FUNDI WAKE KAMSHAURI TAFUTA BOYA UMSHIKISHE.
Kununua gari lililotumika bongo ni bahati nasibu (50/50)....Unaweza kula au Ukaliwa..
Unaponunua gari lililotumika bongo unatakiwa uangalie mambo mengi sana kwa sababu hapa ni sawa na kubet..
Kwanza usipende kununua gari lililooshwa injini mchana na wewe ulinunue jioni, pengine kuna sehemu nyingi zinavuja oil hivyo wameosha ili kumhadaa mteja.
Washa injini, itapendeza zaidi kama injini itakuwa imepoa yaani gari halijaendeshwa kwa muda wa masaa sita na kuendelea....hii itasaidia kuona uwakaji wa injini ni wa kulazimisha au inawaka kawaida, je ikishawaka RPM ipo ngapi, na RPM inashuka kwa wakati na kufikia kiwango kinachohitajika..?Je sailesa yake ikoje, ipo rafu au imetulia?Je unapowasha hakuna pipe yoyote inayovuya aidha hewa, maji au oil..?
Je unapowasha moshi wake ukoje, mweupe au wa blue kwa gari za petrol...kama ni mweupe kama mvuke basi gari linaunguza coolant kwenye combustion chamber, kama ni wa blue basi linaunguza oil.
Je inji inatetemeka?Hapa yaweza kuwa misfiring au Mounts zimechoka..
Injini inapokuwa ON, je bado kuna taa za tahadhari zinaendelea kuwaka kwenye dashboard..? Kama zipo je ni zipi?
Kagua sehemu za chini zenye maungo yanayozunguka kuona kama kunavuja grease au oil kwa mfano Boots za CV joints..
Na ukiridhika kununua gari kwa mbongo, liendeshe kwa umakini kwenye barabara mbovu ambayo si lami...hii itakusaidia kusikia kama kuna sehemu zinagonga gonga na kama una utundu wa magari utagundua kuwa milio inayotoka ni major issues au minor issues..
Washa gari sehemu ambayo ni tambarare, kama ni auto weka D kisha achia brake usikanyage mafuta...Gari likiondoka taratibu ni ishara kuwa gear box bado nzima... (hii si guarantee)....likikataa kuondoka mpaka ulazimeshe kwa kukanyaga mafuta, basi gear box imeanza kuchoka.
Endesha gari hilo kwenye high way ili uone uchanganyaji wake, kwenye miinuko ya kawaida jaribu kuona kama lina pooling ya kufikia angalau speed 100.
Kagua ubora wa body, je imerudiwa rangi au haijarudiwa., kama imerudiwa rangi penda kujua ni kwa nini, huenda gari lilipata ajali..
Kaguq mambo mengine madogo madogo mfano AC, Wiper, Power Windows,Power mirror na kadhalika...
###$$$&&&....Endapo umekagua mambo hayo na ukaridhika na ukaamua kununua gari husika, lioeleke garage....Mwaga injini oil weka unayoiamini, badili Spark plugs, badili air filter kama imechoka, badili fuel filter, badili transmission fluid na uweke uliyopendekezwa.....Kwa nini ufanye yote haya..? Ni kwa sababu hujui mtumiaji wa awali alikuwa anafanya service za uhakika au laa..
Mwisho kabisa peleka gari CAR WASH likaogeshwe kuondolewa gundu....pengine gari hilo lilikuwa linatumika kuchepukia na wake za watu...yaani ni guest house...
Au litakase kwa imani yako coz wengine wanazindika magari yao kwa waganga..
Hii ndiyo BONGO...[emoji847][emoji847][emoji847][emoji847]
Sent using Jamii Forums mobile app
Habari zenu,
Aisee ni vitu gani muhimu vya kuangalia wakati nachukua gari jipya au lililotumika?
Darsa swafi,ila kuna mwamba alinunua gari mpya kabisa 0 km.sasa akalepeka tena gereji nikamuuliza kwa nini?akanambia ameenda kitoa thermostat,
Sent using Jamii Forums mobile app
Bora nidundulize niagize mtumba kutoka nje au ninunue mtumba showroom hapa bongo kuliko kumvua m-bongo mwenzangu...haya mambo unaweza kufa kwa pb
Sent using Jamii Forums mobile app