Unaanzaje kuoga maji ya baridi asubuhi na kuna baridi?

Ha ha haa aisee kweli we ulizoea. Mimi mpk leo naogopa maji baridi asbh
 
Dah! Umenikumbusha pale NJOSS, mwezi wa sita halafu ukiingia darasani, viti vina top ya bati. Ni hatari tupu...
dah mmenikumbusha mbali sana...mm nilipofika njoss nilijifanya naoga kila siku asubuhi lkn ilipofika mwezi wa 6 kwa mara ya kwanza nilimaliza siku 30 ktk maisha yangu kwa mara ya kwanza bila kuoga..ulikua ni mwendo wa paspot size tu
baridi ya njombe ni jipu
 
Dah!.. siku 30 mkuu... ni hatareee sana hiyooo!....
 
Ni bomba sana kuoga maji ya baridi kwa afya yako, shughuli ni sekunde 30 za mwanzo lakini baada ya hapo mwili unakuwa umesharidhia hivyo unaweza kuendelea kuoga bila shida wengine hudai kuanza na maji ya moto kwa sekunde chache kisha kubadili na kuhamia maji ya baridi.

Mimi huwa nahesabu moja, mbili, tatu naingia mzima mzima na kwa vurugu utadhani vita.
 
Kwenu hakuna hata heater za kuchemshia maji kwenye msimu wa baridi?Au jiko la umeme mbona fasta tu.
 
Nakumbuka kigoma Huko Kambini Mtabila jirani kidogo na Burundi kuna Baridi kama Lote mpaka viganja havikunji vinabaki kukakamaa...

Basi hapo sijaoga siku Nne, ile ya Tano kwa aibu ndio nqingia Bafuni baridii la hatari Basi naanza kutukana mitusi huku naoga mixer mikelele ya ovyo ovyo.

JkT kutamu.
 
Unaanza kunawa miguu mpaka mapajani,halafu unanawa mikono mpaka mabegani,halafu unatia maji kichwani then unainuka haraka haraka halafu unachota tena maji unajimwagia fasta mwaaa hapo itakuwa umeshamaliza tatizo.
 
Unaanza kunawa miguu mpaka mapajani,halafu unanawa mikono mpaka mabegani,halafu unatia maji kichwani then unainuka haraka haraka halafu unachota tena maji unajimwagia fasta mwaaa hapo itakuwa umeshamaliza tatizo.
Hahahaha we jamaa bwana unaanzaje mapajani aisee wkt huko ndio kuna ile joto ya sentigredi 36?
 

Kama unaoga kutoka kwenye karai au ndoo; chukua bakuli lenye ukubwa wa kutosha au tumia mikono yako kuchota maji ujimwagiae kichwani na mabegani. Kama unaoga kutoka bafu la mvua, basi fungua bomba kusudi mvua ianze kunyesha kwanza halafu uingie kunyeshewa, na kama unatumia bafu la kuzama au uko kwenye bwawa kubwa wewe zama tu ndani ya maji. Nadhani nimekusaidia sana lazima unipe like hapa; ama sivyo hakieleweki!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…