Unabii juu ya tawara zote duniani,Tanzania kuwa jiwe kuu la pembeni.

Unabii juu ya tawara zote duniani,Tanzania kuwa jiwe kuu la pembeni.

ONJO

JF-Expert Member
Joined
Jun 1, 2022
Posts
216
Reaction score
265
.
Sauti ya kilio na maombolezo ilisikika watu wasikubali kufarijiwa kwa kuwa hayupo tena,amelala.

Siku zikapita,miezi ikapita,na hatimae mwaka ukapita nisielewe maana ya fumbo hili!.Nikijiuliza kwanini ardhi imekubali kumpokea wakati bado tunamwitaji?

Nikiwa katika usingizi,tazama nilikuwa nimekaa katika giza nene!.Mara nikaona nyota iking'ara kupita zile zingine zote na zile nyota zikaanza kuizunguka ile nyota,nikaitazama na ghafla ikatoweka kukawa na giza kuu,huzuni ikatanda ndani ya moyo wangu.

Nikiwa katika kufikili maana ya fumbo hilo,nikaona Nyota mbili;moja ikitokea Mashariki na ile nyingine ikitokea Magharibi; zikijongea(kutembea) kwa kuelekeana na badae ziligongana uso kwa uso na kuwa Nyota moja yenye kutoa nuru kubwa kuliko ile ya kwanza.

Mwanga wa nyota hii ulikuwa mkubwa kuliko ule wa mwanzo, wala mawingu hayakuweza kuuzuia kutoa mwanga wake.

Ndipo nilipomkumbuka yule mteule na hadithi yake,inayohusu kumchukua Binti mrembo aliyekuwa anaishi juu ya mlima;wala hakupatikana mtu wa kumchukua isipokuwa kijana mdogo.

Nikauliza ni nani huyo Bwana uliyemchagua?.Akaniambia utakapomwona Rais Samia S Hassani katoka madarakani,kiti cha Raisi kitachukuliwa na Kassimu majaliwa;na uongozi wake utakuwa mkali sana.

Tena nikaona Malaika toka pande zote za mbingu na watu wote wa Dunia wakimtazama yeye aliyechaguliwa.Nami nikasema sasa Hasira ya Bwana inatulizwa kwa sababu ya kiongozi ambaye moyo wake umempenda upeo.

Nanyi ndugu muonapo ishara hizi zikitokea,Aminini kuwa Mungu humwinua mtu ampendae kwa wakati wake.
 
Anaandika ONJO katika nchi ya walio hai.Upendo wa Mungu wetu na uwe nasi siku zote.

Mambo yale aliyoyaona na kuyaandika Daniel mtumishi wa Mungu juu ya tawala za wakati ule na ujao baadhi yalitimizwa na mengine bado hayajatimizwa mpaka sasa.Mambo hayo aliyoyaona Daniel alioneshwa pia Yohana kipenzi na mwanafunzi wa Bwana wetu Yesu kristo.Ndugu zangu habari ya mambo hayo ni kweli.

ijulikane kwambo tokea kwa Musa mtumishi wa Mungu hakutokea tena mfalme kama Sulemani mwenye Hekima mpaka kuja kwa Yesu.Na baada ya Yesu kunyakuliwa mawinguni hakuna kiongozi aliethubutu kutawala kwa kutumia mafundisho Yesu.Mpaka sasa serikali zote duniani zimeangamia kwa kukosa ufahamu.

Angalia hapa
1.Serikali zinahukumu watu.Kunyongwa,jela miaka 3 0 na adhabu zingine.(mth 7:1,msiwahukumu wengine msije nanyi mkahukumiwa)
2.Uwepo wa makanisa mengi.
Siku izi kuna wachunguji ambao wanapotosha watu wengi,wakifunika fahamu zao za kufikiri kwa miujiza ya ajabu.Mfano kupakwa mafuta,mifungo isiyo na maana,kulialia wakisingizia wameshukiwa na roho mtakatifu.Baadh yao wameacha kufanya kazi kisa maombi.Dunia imeharibika

3.Ubaguzi wa rangi kimataifa,uwepo wa umoja wa waafrika(AU) Na umoja wa watu wa ulaya(EU) kwa lugha nyepesi kuna Dunia ya watu weusi na Dunia ya watu weupe.Tumeangamia
4.Mikataba ya ajabu.Mfano Tanzania na DP word ya dubai,ni wa hiari lakini kwenye kuuvunja kuna gharama tangu kale hakuna free will,ambayo ndiyo yenye maana kwa ufalme wa mungu.Mataifa yamepotoka.
5.Amani na upendo vimetoweka,dunia kwa ujumla hasa nchi za magharibi.
6.Ukosefu wa haki sawa.Mfano Tanzania CAG anatoa taarifa za ulaji wa pesa serikalini lakini hakuna hatua yeyote inayochukuliwa.Wakati huo kuna watu wanafia jela je kuna haki
hapo!(wanaoiibia serikali ni akina nani mpaka waachwe?).Mataifa yote yamepotoka

CORONA ilikuja kutufundisha kidogo ili tumgeukia Mungu lakini mataifa yote hayakusikia wa kutubu badala yake wameendekeza ushoga,wanawake bandia na maovu yote.Hakika tumeangamia

UJUMBE WA KINABII NI HUU HAPA KWA MATAIFA YOTE

1.Mungu ataanzisha ufalme mwingine.
Daniel 7:25-27,huyo atamkufuru Mungu(mnyama wa nne) mkuu na kuwatesa watakatifu wake.Atajaribu kubadilisha nyakati na sheria zao,watakatifu watatiwa mikononi mwake kwa mda wa miaka mitatu na nusu.Lakini mahakama itafanya kikao;watamnyang'ana utawala wake,nao utafutwa na kuangamizwa kabisa.Ufalme,utawala na ukuu wa falme zote duniani watapewa watakatifu wa mungu mkuu.
Ufalme wao utakuwa wa kudumu milele na tawala zote zitawatumikia na kuwatii.

2.Mungu atatuma habari njema tena.
Ufunuo 14:6-7,kisha nikamwona malaika mwingine anakaa juu angani akiwa na habari njema ya milele ya mungu aitangaze kwa watu waishio duniani,kwa mataifa yote na watu wa lugha zote na rangi zote,naye akasema mcheni mungu na kumtukuza maana saa imefika ya kutoa hukumu yake,mwabuduni yeye aliyeumba mbingu na nchi Bahari na chemichemi za maji.

3.Atatawala kwa fimbo ya chuma.
Ufunuo 19:11,12,15 kisha nikaona mbingu zimefunguliwa,na huko alikuwepo farasi mmoja mweupe na mpandafarasi wake aliitwa ''mwaminifu na kweli''huyo huhukumu na kupigana kwaajili ya haki,alikuwa amevaa vazi lililolowekwa katika damu na jina lake ni ''neno la mungu''(second Jesus).Yeye ndiye atakaye tawala kwa fimbo ya chuma na kuikamua divai katika chombo cha kukamulia zabibu za ghadhabu kuu mungu mwenye nguvu.

4.Atavikwa taji ya kuwa Mfalme wa wafalme na Bwana wa mabwana.
Ufunuo 11:16,juu ya vazi lake,juu ya paja lake alikuwa ameandikwa jina''Mfalme wa ufalme na Bwana wa mabwana.

HAYO YOTE YATATIMIA LINI?

Niliwahi kuandika uzi unaosema ''lipo tumaini kwa watanzania na dunia kwa ujumla''

hapo kwa uweza wa mungu mkuu,nilitabiri viongozi watakaokuja baada ya Mh.Samia Suluhu Hassani Raisi wa Jamhuri ya muungano wa tanzania,akitoka madarakani.Atafatiwa na Kassimu Majaliwa ambae kwa sasa ni waziri mkuu wa nchi.Mnaweza mkaona kumbe mambo haya yatatimia katika awamu ya nane.Huyu ndiye atakuwa kiongozi atakayebeba sifa zote hapo juu.

Yaani
1.Amebeba habari njema
2.Jina lake ni neno la mungu kwa kuwa ana ujumbe wa mungu.
3.Atawaangoza mataifa kwa fimbo ya chuma.
4.Atapewa kila aina ya heshima kwa sababu uweza wa mungu upo na yeye.


Mataifa yote duniani furahini pamoja nami kwakuwa nimewaleteeni habari njema ya wokovu.Nao ufalme wa mungu umekaribia.

Wanaheri wote watakaoiona siku hiyo ya ujio wa mwana wa mtu.

Na ONJO Mpenzi wenu.
Umesema vema ✔️. Ila hapo Kweny DP world umeyakanyagaa... Utashambuliwa hapa na wazee wa posho za kupush agenda ya DP world vibaya mno!!
 
Back
Top Bottom