Unabii unavyotumika vibaya Tanzania

Unabii unavyotumika vibaya Tanzania

Victor Mlaki

JF-Expert Member
Joined
May 1, 2016
Posts
4,151
Reaction score
4,277
Naandika kwa masikitiko makubwa sana juu ya uchuro unaofanywa na watu wanaojiita manabii katika Nchi ya Tanzania. Bila shaka nimefuatilia uchuro mwingi sana jambo ambalo nimeona siyo vyema kuacha kuandika ili kama wapo humu waelewe tumeshawagundua na jambo la msingi zaidi waache uchuro ili unabii wa kweli ufanye kazi yake.

Kumekuwa na utitiri wa manabii uchuro kuliko manabii halisi katika Nchi ya Tanzania jambo ambalo likiachiliwa na kuendelea kushamiri yatajirudia yale yaliyowapata wafuasi wa Kibwetere. Hivyo,basi kabla hawa wachuraji hawajafika mbali zaidi ni zikachukuliwa hatua za mapema za tahadhari "proactive measures".

Viongozi wakubwa wa kisiasa wamekuwa wakichuriwa vifo na manabii uchuro kila uchao. Unabii umekuwa ni wa kutabiri juu ya mabaya yatakayoyokea kuliko mazuri. Swali la kujiuliza kimyakimya ni je, hawa manabii wao huoneshwa mabaya tu na siyo mazuri?

Kuna nabii mmoja nimefuatilia maelezo yake kwa karibu leo nikacheka sana kwa sababu ni usanii mtupu anafanya halafu watu wanamtumia pesa na kumuita MTUMISHI wa Mungu. Kibaya zaidi anajipa sifa kama kawaida yao ilivyo na kusema ana sifa nabii bora katika Tanzania kama alivyo Mtu wa Mungu T.B Joshua. Ametabiri kuwa ndani ya mwezi huu wa tatu na ukipita basi wa tisa kuna Kiongozi mwingine mmoja ambaye akisimama ana alama mwilini tofauti na wenzake na jina lake ni namba tano yupo kwenye hali ngumu tumuombee sana na akaahidi ana package nyingine ataisema siku nyingine. Hawa jamaa wanacheza sana na mashaka ya watu juu ya jambo na kutumia mwanya huo kama fursa ya kuongeza hofu zaidi kwa watu ili kujinufaisha wao.

Hawa jamaa wanafahamika sana na kuna watu wameshatiwa sumu akilini na hawa wasanii ndiyo wanaowafanya kuwa na kizuri cha kuendelea kutumia mashaka na tashwishwi za watu juu ya wakati ujao kama njia ya wao kuzidisha hofu na ujinufaisha.

Hawa watu wanapaswa kulipa kodi kutokana na biashara wanyoifanya ili angalau kila fursa inayopatikana nchini ilifaidishe Taifa hili. Kama wafanyabiashara wadogo wanaotafuta shilingi Mia Mia kila siku wanaolipa kodi hawa wanaobumbabumba mambo na kutumia milioni moja, mbili n.k nao walipishwe kodi ili mapato ya Taifa hili yatufaidishe wote.

Nina uhakika hawa manabii uchuro wakilipishwa kodi litakuwa ni jambo zuri sana kwa sababu watakuwa wamempa pia Kaisari haki yake kama wanavyojibainisha kuagizwa na Mungu.
 
Ata humu JF kila mtu ameanza kuandika pumba akizamilia yatokee badae apate credit.
 
Ata humu JF kila mtu ameanza kuandika pumba akizamilia yatokee badae apate credit
Hapo kwenye kila mtu embu fafanua kidogo Mkuu. Sioni link ya kuandika pumba na unabii uchuro.
 
Mie naona unawaita wachuro kwa sababu wameongea usichotaka kukiskia, nina uhakika kuna watu wanafurahishwa na kazi ya wachuro na ukiona mtu anafurahia mambo mabaya juu ya hao unaowaita viongozi basi wanapaswa kujitathmini mienendo yao
...
 
Swali la kujiuliza kimyakimya ni je hawa manabii wao huoneshwa mabaya tu na siyo mazuri?
Wale wa kanisani kwangu wenyewe huwa wanatabiri kulingana na tetesi. Zikishavuma tetesi kwenye mitandao halafu pengine kuna baadhi ya watu wakawa wamezathibitisha, basi anainuka nabii na kutioa utabiri watu waombe juu ya unabii anaoutoa. Kwa ujumla kanisani kwangu hakuna nabii na ninadhani kwa mazingira yaliyopo kwa sasa, hatakuja teana kutokea kuwepo nabii wa Mungu mahali pale
 
Halafu ingekuwa na maana kama wanapooneshwa wangekuwa wanaomba na kumsihi Mungu aghairi mabaya kama iwapasavyo Watakatifu wa Bwana.

Kwanini wanashindwa kuomba kumsihi Mungu kugairi mabaya?

Yani hawa jamaa wanashangaza sana aisee unless hawajamfamu Roho wa Mungu vizuri.
 
Namuona Vice president Mzee Mtu mzima anayevaa miwani akiapishwa na Mama Samia.
 
Vijijini ni hatari kwa hawa manabii wenye smartphone na wenye uwezo wa ku"google"..niliwahi kusikia unabii mahali fulani Nyamtengera huku ninatamani kulia.
 
Jambo likisemwasemwa sana hatimaye huwa kweli. Utabiri ni ubashiri. Unaweza kuwa ama usiwe na huwa hauna kikomo cha muda.
Hiki unachosema wewe ni mass energy. Hii kitu ina nguvu sana na sometimes kwa uchache sana lakini inaweza kuathiri maamuzi ya kiroho.
 
Jambo likisemwasemwa sana hatimaye huwa kweli.. Utabiri ni ubashiri. Unaweza kuwa ama usiwe na huwa hauna kikomo cha muda...
Hiki unachosema wewe ni mass energy. Hii kitu ina nguvu sana na sometimes kwa uchache sana lakini inaweza kuathiri maamuzi ya kiroho
Asante sana kwa ufafanuzi mzuri.
 
Back
Top Bottom