Unachukua hatua gani biashara inapodorora?

cold water

JF-Expert Member
Joined
Oct 6, 2021
Posts
238
Reaction score
954
Nimeanzisha biashara ya bisi(popcorn) kwa packaging lakini inaenda wiki mbili sasa inatoka taratibu sana na siku nyingine haitoki kabisa. Nichukue hatua gani maana nategemea nipate faida ili niendeshe maisha. Najikuta nakula tu hela inayopatikana kidogo kama ni 1000/= naipigilia tu, yani I wish ingekuwa inakaa ndani ya siku 2 iwe imeisha ili faida nifanyie matumizi mtaji ubaki lakini wiki 2 biashara gani hii.

That s why sipendagi hizi biashara ndogo ndogo zenye faida ya 500 kwa mtaji. Nawaza nianzishe hata karanga vipi nazo zisipotoka?
 
Nimeanzisha biashara ya bisi kwa packaging lakini inaenda wiki mbili sasa inatoka taratibu sana na siku nyingine haitoki kabisa nichukue hatua gani mana nategemea nipate faida ili niendeshe maisha.
Tembeza mitaani mazee, ongeza ubunifu.
 
Kwanza nakuonya kudharau biashara yako uache tabia ya masihala.Je kabla hujaanya biashara ulifanya uchunguzi a soko?Usikate tamaa wiki2 ni ndogo kujuwa kama mahala panabiashara au hakuna vuta subira zaidi.
 
Kwanza ilipaswa utuombe ushauri kabla ya kuanza hiyo biashara au ungetueleza msukumo uliokupelekea kuanzisha hiyo biashara.

Huwezi kulazimisha mvua za kutosha zinyeshe kipindi cha Kiangazi.
 
Kwanza kabisa Hongera kwa Kuanza.
Weka nguvu nyingi sana kwenye Marketing, Marketing, marketing. Hakikisha wanakujua Wewe na Bidhaa zako

Nicheki Wasap nikupe marketing tips: 0714453664
Njoo na vocha ya buku 5
 
Usiogope,watakwimu wanasema ktk biashara (ndogondogo) 10 zinazoanzishwa kwa mwaka,basi 7 hufa na 3 ndo hudumu.Hii inaonyesha haupo peke yako mara ukaanza kujidharau.

Nikukmbushe kuwa kosa kubwa unalolifanya ni kuitegemea biashara wakati yenyewe haijajitegemea.Na hili ndo huwaangusha wajasilia walio wengi.

kwo jitahidi uongeze mtaji lakini katika mtaji huo tenga na pesa ya kula(yaani inaitwa nguvu kazi) ili badae ukishazalisha basi uanze kula faida na siyo kuugusa mtaji!
 
Mtandao wa Investopedia ulitoa sababu ya biashara ndogo kufa, 1. Mtaji Mdogo, 2. Uendeshaji Mbovu, 3. Mpangilio Mbovu wa Biashara na Bidhaa yako au huduma yako haihitajiki sokoni (Hakuna wateja wanahitaji bidhaa zako). Pamoja na sababu zingine nyingi.
 
Apo unapotengenezea bis usiache sku nzma bila kukaanga wngene ununua wakisia harufu weka hata kias kidogo jkon za kuchangamshia eneo pili watu wakiwa wanapta chota kias kuonjesha hasa watoto wakiwa na wazaz au watu wazma lazma utaauza tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…