Unyanyasaji wa kijinsia mtandaoni (OGBV) ni aina ya unyanyasaji unaofanyika kupitia teknolojia na intaneti. Unahusisha mtu au kundi la watu kutumia njia za mawasiliano ya kidijitali kuwaumiza, kuwadhalilisha au kuwasumbua wengine kwa misingi ya jinsia zao au sifa nyingine, kama vile mwelekeo wa kingono na mwonekano wao.
Unyanyasaji huu ni mwendelezo wa ubaguzi wa kijinsia unaotokea katika maisha ya kawaida, lakini unapofanyika mtandaoni, athari zake huongezeka na kusambaa kwa haraka.
Baadhi ya matendo yanayohusishwa na Unyanyasaji wa Mtandao ni pamoja na kutuma jumbe za vitisho, matusi, kusambaza taarifa binafsi, maudhui ya kingono, Kutumia mifumo ya GPS kumfuatilia mtu bila ridhaa, kuwadhuru wengine.
Kwa mujibu wa ripoti ya Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) 2025 matukio ya uonevu mtandaoni yaliyoripotiwa yalipungua kwa asilimia 55.2 kati ya mwaka 2023 na 2025, kutoka matukio 475 hadi 213.
Soma Makosa ya Uonevu na Unyanyasaji Mtandaoni yapungua kwa 41.3% nchini (2022–2025)
Kwa upande wa jinsia, wanaume walikuwa na idadi kubwa zaidi ya wahanga walioripotiwa kuliko wanawake katika kila mwaka kuanzia 2022 hadi 2025.
Mwaka 2025, wanaume walikuwa 161 (asilimia 75.6), huku wanawake wakiwa 52 (asilimia 24.4) kati ya jumla ya wahanga 213 walioripotiwa.
Lakini swali linabaki: Ni vitu gani vinachochea unyanyasaji wa kijinsia mtandaoni?
- Je, ni ukosefu wa sheria kali?
- Je, ni Makuzi?
- Je, ni Utamaduni?
- Je, ni Mazoea?
- Je, ni Hulka?
- Je, ni utofauti tu wa mitazamo?
- Je, ni ukosefu wa Elimu?
- Je, ni watu kutojiheshimu?