Wild Flower
JF-Expert Member
- Jul 20, 2023
- 378
- 766
Jiji la Dar es Salaam lilianza kama Kijiji kidogo cha wavuvi kilichojulikana kama Mzizima. Kijiji hiki kilianzishwa na Wabalawa ambao walichanganyika na Wazaramo kuelekea kwenye maeneo ya Bara la Afrika Mashariki na ambazo zilijulikana kama ‘Caravan Routes’. Ujenzi wa Makao ya Sultani pamoja na bandari ulianza rasmi mwaka 1865 katika eneo la kijiji cha Mzizima. Ujenzi huo ulikamilika mwaka 1866 na Sultani Majid bin Said kuhamia Dar es Salaam mwaka huo.
Mara baada ya Sultani Majid bin Said kuhamia Dar es Salaam mji ulianza kupanuka na uchumi wake kukua kwa kasi kubwa japo kwa kipindi kifupi ambapo Sultani Majid bin Said alifariki mwaka 1870. Kifo cha Sultani huyo kilisababisha kudidimia kwa maendeleo ya mji wa Dar es Salaam. Hali hiyo ilianza tena kubadilika mwaka 1884 kufuatia kuanzishwa kwa koloni la Wajerumani la Afrika Mashariki. Mwaka 1886 jiji hili lilipewa jina la 'Daresalaam' ikimaanisha "Bandari Salama",
Mwaka 1891 Serikali ya kikoloni ya Kijerumani iliamua kuhamisha makao makuu ya utawala wake katika Afrika Mashariki kutoka Bagamoyo na kuyaweka Dar es Salaam. Hata hivyo, baada ya Wajerumani kushindwa na Waingereza katika Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia mwaka 1916, Mji wa Dar es Salaam uliendelea kuwa makao makuu ya utawala wa koloni la Waingereza nchini Tanganyika hadi ilipojipatia uhuru wake mwaka 1961. Dar es Salaam iliendelea kuwa makao makuu ya Tanganyika huru na hatimaye kuwa makao makuu ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania hadi mwaka 1972 wakati Serikali ilipoamua kuhamishia makao yake makuu mjini Dodoma. Jiji la Dar es Salaam liliendelea kubaki kuwa maarufu kwa kuwa Jiji kuu na kitovu cha biashara nchini Tanzania.