Unafahamu toba ya uzinzi na uasherati?

Unafahamu toba ya uzinzi na uasherati?

neno ni upanga

JF-Expert Member
Joined
Jun 28, 2022
Posts
494
Reaction score
1,656
Habari wakuu!!

Wote tunaamini ipo siku tatasimama mbele za Mungu kutoa hesabu ya yale tuliyoyafanya, mambo ambayo yatatupa uhalali wa kuingia mbinguni au kukataliwa na kutupwa kwenye ziwa la moto! Mtu haendi motoni kwa sababu amefanya dhambi ila anaenda motoni kwa sababu amekataa kutubu hiyo dhambi na hata kama alitubu basi alitubu vibaya!

Kila dhambi ina toba yake na jinsi inavyotakiwa kutubu na toba ya mhusika kukubaliwa
Leo tutaangalia dhambi ya uzinzi na toba yake

1: Ikiwa wewe ni mwanaume na umeoa na ukazini na mwanamke mwingine ambaye hajaolewa

Toba yake ndo hii
Nenda kwa mke wako kamuombe msamaha (Ungameni dhambi zenu ninyi kwa ninyi, na kuombeana, mpate kuponywa. Kuomba kwake mwenye haki kwafaa sana, akiomba kwa bidii. Yakobo 5:16)

Baada ya hapo nenda kwa mchungaji wako akuombee baada ya hapo nenda mbele za Mungu umuombe msamaha!

Afichaye dhambi zake hatafanikiwa; Bali yeye aziungamaye na kuziacha atapata rehema.

Mithali 28:13

Na kama umezini na mke wa mtu mtafute mme wake muombe msamaha maana umemtendea ubaya huyo mwanaume kwa kulala na mke wake!

2: kama wewe ni mwanamke umefanya umezini fanya kama nilivyoeleza hapo juu, ndipo msamaha wako utapokelewa

kuingia mbinguni kunahitaji gharama ambayo wakati fulani lazima uaibike au hata kuwa mjinga ili uuingie ufalme wa Mungu!! Ni bora kuabika ukiitafuta mbingu kuliko kwenda kuchemka motoni milele

Note Afichaye dhambi zake hatafanikiwa; Bali yeye aziungamaye na kuziacha atapata rehema.

Mithali 28:13
 
mungu anatumia muda wake kutuumba, anatupa uwezo wa kufanya dhambi alafu mwisho wa siku tukifa anatutupa kwenye ziwa la moto, mbona kama anafanya mchezo wa kikatili hivi???!! kisa tu anataka kuabudiwa!!!
 
Akili mtu wangu

Umetembea na mke wa mtu alafu umuombe msamaha mme wake? Are you serous? Unatengeneza nini hapo? Unafikiri utaachwa? Toba inahitaji busara. Mungu ni Mungu wa Amani. Usimwendee mwenye mke, muombe Mungu msamaha tu na kuacha kabisa jambo hilo
 
Ha
Habari wakuu!!

Wote tunaamini ipo siku tatasimama mbele za Mungu kutoa hesabu ya yale tuliyoyafanya, mambo ambayo yatatupa uhalali wa kuingia mbinguni au kukataliwa na kutupwa kwenye ziwa la moto! Mtu haendi motoni kwa sababu amefanya dhambi ila anaenda motoni kwa sababu amekataa kutubu hiyo dhambi na hata kama alitubu basi alitubu vibaya!

Kila dhambi ina toba yake na jinsi inavyotakiwa kutubu na toba ya mhusika kukubaliwa
Leo tutaangalia dhambi ya uzinzi na toba yake

1: Ikiwa wewe ni mwanaume na umeoa na ukazini na mwanamke mwingine ambaye hajaolewa

Toba yake ndo hii
Nenda kwa mke wako kamuombe msamaha (Ungameni dhambi zenu ninyi kwa ninyi, na kuombeana, mpate kuponywa. Kuomba kwake mwenye haki kwafaa sana, akiomba kwa bidii. Yakobo 5:16)

Baada ya hapo nenda kwa mchungaji wako akuombee baada ya hapo nenda mbele za Mungu umuombe msamaha!

Afichaye dhambi zake hatafanikiwa; Bali yeye aziungamaye na kuziacha atapata rehema.

Mithali 28:13

Na kama umezini na mke wa mtu mtafute mme wake muombe msamaha maana umemtendea ubaya huyo mwanaume kwa kulala na mke wake!

2: kama wewe ni mwanamke umefanya umezini fanya kama nilivyoeleza hapo juu, ndipo msamaha wako utapokelewa

kuingia mbinguni kunahitaji gharama ambayo wakati fulani lazima uaibike au hata kuwa mjinga ili uuingie ufalme wa Mungu!! Ni bora kuabika ukiitafuta mbingu kuliko kwenda kuchemka motoni milele

Note Afichaye dhambi zake hatafanikiwa; Bali yeye aziungamaye na kuziacha atapata rehema.

Mithali 28:13
neno ni upanga naomba kuuliza maswali kutokana na maelezo haya, mwizi kabla hajaomba msamaha kwa Mungu inabidi amuombe aliyemuibia? na muuaji je? atamuomba nani?
 
Back
Top Bottom