Unafaidika na nini ukifanya mazoezi ya Kutembea au Kukimbia?

FikraPevu

JF-Expert Member
Joined
Jan 2, 2010
Posts
304
Reaction score
236
Watu wanaofanya mazoezi ya kukimbia na kutembea wana mambo mengi yanayofanana. Wote wanatumia njia mbalimbali kufikia malengo ya kuimarisha afya ya mwili.

Changamoto inajitokeza ni kwenye faida na hasara za mazoezi ya kukimbia au kutembea ambapo kila kundi lina hoja zake ambazo zinatofautiana na kundi lingine. Wakimbiaji wanafikiri kukimbia kunachoma mafuta haraka, kuongeza mzunguko wa damu na kumaliza haraka mazoezi. Watembeaji wanasema athari za viungo vya mwili ni ndogo, mapigo ya moyo huenda vizuri.

Njia ya kuondoa utata kwa makundi yote mawili ni kuwaruhusu wataalamu wa mazoezi kushauri faida na watu gani ambao wanastahili kukimbia au kutembea kulingana na afya ya mtu.



Mazoezi ya Kutembea

Kutembea kunaepusha madhara mbalimbali ikiwemo majeraha ya magoti, kiuno na nyonga. Kukimbia kunatumia nguvu nyingi za kukanyaga ardhi na kusababisha msuguano kwenye mifupa na muunganiko wa mifupa kuliko mazoezi ya kutembea.

Pia kuna muunganiko thabiti wa akili na mwili wakati wa kukimbia. Hata hivyo, kukimbia na kutembea kunaimarisha afya ya akili lakini kutembea kuna faida kubwa zaidi. Stephanie Powers, Mkufunzi wa Afya ya akili na mwandishi ya kitabu cha Thyroid First Aid Kit, anashauri watu watembee haraka na kurusha mikono ili kufaidika zaidi.


Mazoezi ya Kukimbia

Haina mjadala kuwa kukimbia kunachoma zaidi mafuta ya mwili kuliko kutembea. Daktari Patrick Suarez, Mtaalamu wa afya ya Mifupa ameliambia Jalida la POPSUGAR kuwa mafuta ya mwili yanachomwa mara mbili zaidi kwa wakimbiaji kuliko watembeaji kwasababu kiwango cha mapigo ya moyo huongezeka maradufu.

Ikiwa lengo lako ni kupunguza uzito wa mwili basi kukimbia ni njia rahisi kuliko kutembea ambayo hutumia muda mrefu kuchoma mafuta.

Sio tu wakimbiaji wanachoma mafuta mengi, lakini kukimbia kunatengeneza homoni ya peptide YY, ambayo inawasaidia kutumia mafuta kidogo baada ya mazoezi. Kulingana na utafiti uliofanywa na Chama cha Fiziolojia cha Marekani (2008) unaeleza kuwa kukimbia kunazuia mafuta kutumika kwa wingi mwilini.


UAMUZI

Ikiwa unafanya mazoezi ya kutembea au kukimbia unaweza kuendelea nayo ili kupata faida zilizoainishwa hapo juu. Kulingana na Jo-Ann Houston, Mkuu wa Mafunzo wa kampuni ya GYMGUYZanasema jambo la muhimu ni kutambua na kufurahia faida za muda mfupi na muda mrefu za kila zoezi unalofanya.

Ikiwa ndio unaanza kukimbia au kutembea, chagua zoezi ambalo litakufanya ujisikie vizuri kulingana na mwili wako na malengo unayotaka kuyapata. Jaribu kukimbia na kutembea ili kufanya uchaguzi sahihi wa aina ya mazoezi yanayokufaa. Muhimu chagua zoezi ambalo utadumu nalo muda mrefu.


Zaidi, soma hapa => MAZOEZI: Kutembea au kukimbia? Wataalamu watoa neno | FikraPevu
 
Naomba kujua kiafya mtu anatakiwa akimbie kilometer ngapi kwa siku, nasisitiza KIAFYA. Shukrani
 
Ili uwe gentomen piga km 10 kwa siku, piga pushap walau 300+
Kula ugali Samaki achana na chips

Kila nguo itafit kwako akili itakuwa active
Khaaaa hizooozote namaharii AMA mazoezi
 
Naomba kujua kiafya mtu anatakiwa akimbie kilometer ngapi kwa siku, nasisitiza KIAFYA. Shukrani
Kilo mita nne asubuhi au jioni
Usikimbie kwa spid sana fanya kawaida
Au zunguka uwanja mara kumi japo inaweza isitimie kilomita nne
Kisha fanya skwashi angalau 50
Kama ni mwanaume push up 100 kwa kuanzia ila kwenye push up usiwe na haraka ngoja kwanza hadi zoezi la kukimbia liwe kubwa zaid na skwashi
Pangilia mlo vizuri usizidishe kukimbia sana maana utachosha miguu na mwli utakuwa dhaifu
 
watu wengi wanafikiri ukifanya mazoezi ya kuumiza mwili zaidi ndio yenye tija zaidi kwa mwili kumbe si kweli.
mwanaume ukiwa unafanya mazoezi ya kutembea kwa haraka barabarani wengi watakuona kama mzembe kumbe yanatija kuliko kukimbia mimbio isiokua na mpangilio kulingana na mwili wako. kuna tofauti kubwa kati ya adhabu na mazoezi unaweza ukapoteza muda mwingi ukidhani unafanya mazoezi kumbe adhabu.
 
unatakiwa kufanya mazoezi kwa dakika 45 zoezi lolote lile,kuna kijana mmoja anafika uwanjani saa 12 asubuhi anazunguka uwanja mara 5 halafu anaondoka huyu amekuja kuchekesha mwili haujapata joto hauja anza kuunguza chochote kwenye mwili
 

Shukrani sana kiongozi. God bless you
 
unatakiwa kufanya mazoezi kwa dakika 45 zoezi lolote lile,kuna kijana mmoja anafika uwanjani saa 12 asubuhi anazunguka uwanja mara 5 halafu anaondoka huyu amekuja kuchekesha mwili haujapata joto hauja anza kuunguza chochote kwenye mwili
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]
Anachekesha mwili

Ukute yy ndio hapo anakuw asha pasha
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…