Unafaidika na nini ukifanya mazoezi ya Kutembea au Kukimbia?

Aisee huu uzi ni mfupi unafurahisha ila umeambatana na ukweli.

Napenda sana mazoezi ya kukimbia.
 
Naomba kujua kiafya mtu anatakiwa akimbie kilometer ngapi kwa siku, nasisitiza KIAFYA. Shukrani
Kamikaze in the house, naona wasisitiza KIAFYA [emoji23] [emoji23] [emoji23] Asante baba hutaki shida mjini
 
Naomba kujua wale wenzagu wa martial arts tunakoment wapi maana mazoezi kwetu ni kama msosi ukikosa mwili unasumbua tu.

Angalizo huwa hatujimwambafai, akitokea wa kujimwambafai huyo Mchezo haujui au mgeni.


Mtoa mada asante kwa kutukumbusha faida tuzipatazo.
 
Asubuhi ni muda mzuri sana pia kwa wengi Upata muda huo.

Mimi kila siku naamka saa kumi na moja kasoro naanza kukimbia hadi sasa moja.

Ila Sio constant asubuhi kuna wakati inabidi nifanye mazoezi jioni sababu muda mwingine nakuwa nimebanwa.
kwahiyo mkuu hata ukikimbia asubuhi na jioni ni sawa?
 
Kuna nondo za maana humu kuhusu matizi
Nishachota vipande kazaa vya wadau
Ngoja nisubiri vingine
 
Mkuu umecheza shotogkhan ,taikwando,bujuluu au ipi mda mrefu sana sijapasha even kiki boxing
 
Shotokan kidogo (sipendelei sana karate)
Drunken styles
Thai boxing
Taekwon-do
Capoera (paranawe)
Taichi

Kiujumla boss nimefanya sana mixed martial arts
Nani alikufundisha mkuu?. Au ulijifundisha mwenyewe?
 
Hakikisha japo unafanya mazoezi mara 5 kwa juma,huku uki pumzika siku mbili ila zisifuatane.

Unaweza badilisha aina ya mazoezi kadri hali inavyoruhusu,kama kutembea,kukimbia,kuogelea ama kuendesha baiskeli n.k.

Uwe na mpangilio bora wa Chakula ili kuupa mwili nishati ya kutosha kutokana na mazoezi unayofanya.

Njia iliyo nzuri ambayo itakuwa inakupa hamu ya mazoezi ni kujua lengo lako ni nini hasa,kwa mfano anaye panga kupungua basi ajipime uzito na kuweka adhma ya kupungua uzito alionao kwa kuangalia maendeleo kila mara.

Njia nyingine nikutumia teknolojia ya simu ama saa maalum ambazo hukuwezesha kuona hatua mbalimbali za maendeleo yako ukiwa mazoezini.Kwa mfano kujua mapigo yako ya moyo,umbali gani ume tembea kiasi gani cha nishati umetumia ama kupunguza.

Kuna programu nyingi kwenye Google Store ambazo unaweza kupakua na kuziunganisha na simu pamoja na saa maalum kurahisisha mazoezi kwa ujumla.
 
Kilometa 5+ kwa kukimbia. Kutembea hatua 6,000+. Unaweza kutumia counter ya kwenye simu kujua muda uliokimbia au kutembea kwa wale wenye smart phone.
Nakimbia km 4,natembea km 4,mara 4 kwa wiki,niko vizuri sana kiafya,nimeshuka weight kutoka 85kg sasa niko 72kg na nina umaintain,na ndio uzito niliokuwa nauhitaji,niko vizuri sana kiafya ingawa kabla ya hapo nilidevelop hypertension,kwahiyo nawashauri watu kufanya mazoezi kwa afya bora...
 
Mkuu kama programu ipi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…