Unafanyaje kuendesha biashara ya mtandaoni inayohusisha utoaji wa huduma fulani hasa kwenye uaminifu?

Unafanyaje kuendesha biashara ya mtandaoni inayohusisha utoaji wa huduma fulani hasa kwenye uaminifu?

OgaBoy

JF-Expert Member
Joined
Aug 22, 2022
Posts
1,531
Reaction score
2,140
Assume unatangaza kazi zako kutokea mikoani kwenye social media hupati wateja kwenye mkoa wako, hatimaye wengi hutoka Dar.

Je, unawezaje kuwafanya wakuamini hasa wale wanaohisi kutapeliwa kila siku na huenda washatapeliwa

Je, uhamie Dar wakati bado unajijenga au ufanye kipi? Vipi huko. Baadae wakitokea mkoani ulikohama!
 
Jitahidi wateja wa mwanzoni uwafanyie vyema, watakuletea wapya na kukutetea watu wakihoji uaminifu
 
Assume unatangaza kazi zako
Ila hujatwambia ni kazi zipi.

Kumbuka wako wengi wafanyayo kazi kama yako, ukiitaja hio kazi, nao wengine pia watakuja kutoa ushauri nini wanafanya ili kuwafikia wateja wa mbali kupitia mtandao.

Neno langu kwako ni hili: Fanya kazi kiukamilifu kwa mteja mmoja wa kwanza utakaye mpata, awe wa mkoa wako au mkoa tofauti, huyu mteja mmoja ndio mlango wa kuwafikia wateja wengine, katika mkoa wako, mikoa jirani na hata nje ya nchi.

Mfano hai, Waweza kupitia hii thread yangu: Nunua bidhaa kutoka Mataifa 15 ikiwemo USA, UK, UAE na China sasa
  • Kupitia hiyo thread hakuna mtu ninaye mjua physically au yeye kunijua physically.
  • Kupitia hiyo thread nahudumia watu wa mkoa wangu, mikoani na nchi jirani.
1728795731743.png

Je hadi hapo umejifunza nini?

Nakutakia kheri kwenye kazi yako.
 
View attachment 3123220
Je hadi hapo umejifunza nini?

Nakutakia kheri kwenye kazi yako.
Nimefanyia wengi kwa uaminifu na wengine wamenizurumunmalipo lakini hawa wapya wanaokuja wengi wanauliza location uliwaambia uko sehemu flani wanasema haukizo vigezo vyao kwa sababu ya locationa wengine wanasema wameshatapeliwa hata kama ukiwa pa reference ya wateja uliowapa huduma wakiwa mkoa wao bado hauwaamini. na wengi wao ni makampuni so imekuwa mtu akija ninmpaka awe mwelewa. Otherwise wengine watataka kazi kwanza kisha walipie kulingana na nature ya kazi yangu ni lazima utume malipo ya awali Sasa wale ambao waliwahi kukumbana na dhulma baada ya kutoa kazi na pesa zao wanatianshaka pia kwako, hadi ujirisk utoe pesa Yako mfukoni umpatie huduma kisha alipie baada ya kumkabidhi anapotea pia
 
Otherwise wengine watataka kazi kwanza kisha walipie kulingana na nature ya kazi yangu ni lazima utume malipo ya awali Sasa wale ambao waliwahi kukumbana na dhulma baada ya kutoa kazi na pesa zao wanatianshaka pia kwako, hadi ujirisk utoe pesa Yako mfukoni umpatie huduma kisha alipie baada ya kumkabidhi anapotea pia
Je kwanini hutaki kuweka wazi hiyo kazi yako, ili upewe ushauri stahiki nini cha kufanya?
Assume unatangaza kazi zako kutokea mikoani kwenye social media hupati wateja kwenye mkoa wako, hatimaye wengi hutoka Dar.
Je huoni kuwa unapunguza wigo wa kupata maarifa na ushauri wa kitaalam kutoka kwa wadau wengine wafanyao kazi kama yako
 
Back
Top Bottom