Unafanyaje?

gcmmedia

Member
Joined
Jul 19, 2024
Posts
34
Reaction score
75
Kuna yule jamaa yako, yeye anakupigia simu tu anapohitaji pesa, ukiona simu yake tu, unajiambia “anahiji pesa”, usipompatia anakasirika. Anakulalamikia sana. Yeye anajua una pesa na utampa. UNAFANYAJE na mtu huyu?
 
Binadamu ukimsaidia siku ya kwanza atashukuru, siku ya pili ataweka matumani , siku ya tatu atajua ni haki yake wewe kumsaidia , siku ya nne ukimnyima atakasirika.

Na hapo ndo tatizo linaanzia.

Ila kama ni vielfu mbili mbili vya komoni mpe tu ..Kama unavyo
 
Mi huwa nampa tu ni mwana sana na kinachomgharimu ni ana matumizi makubwa na mkamaria mzuri tu .Pesa zenyewe anazoomba sio kubwa kivile na mshahara kanizidi mbali tu.
 
Mi huwa nampa tu ni mwana sana na kinachomgharimu ni ana matumizi makubwa na mkamaria mzuri tu .Pesa zenyewe anazoomba sio kubwa kivile na mshahara kanizidi mbali tu.
Lannister hamuaminiki kabisa
according to your avatar,
 
Siku nyingine na wewe uwe unampigia na yeye simu kumuomba hizo hela,unamwambia una shida,
Hapo ataelewa tu,
Dont live to impress others,live ur life.

Kama unamsaidia,msaidie tu bila kulalamika,kama unaona ni kero kumsaidia acha,simple tu,maisha ni yako,usijitese.
 
Mwambie hauna pesa kama hautaki kumpa.
 
Mwambie ukweli!

Mimi nilimwambia inawezekana vipi kila ukinipigia simu unaniomba hela? Hamna hata siku moja ya kunijulia hali huu ni urafiki kweli?

Unanihitaji kwenye shida ila ukiwa kwenye raha hata kunijulia hali unashindwa?

Akabaki anacheka na kusema hakuna bhana! Sikumpa hela!

Tangu nilivyomwambia hivyo hajanipigia simu hata ya kunijulia hali tangu mwaka jana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…