Unafanyeje ili usifilisike na usipotee kwenye ramani?

Unafanyeje ili usifilisike na usipotee kwenye ramani?

mwanyaluke

JF-Expert Member
Joined
Jan 22, 2015
Posts
704
Reaction score
2,435
Moja ya mambo yanayotisha sana katika maisha ni kufilisika. Ulikuwa na mali zako kidogo zilizokuwa zinakusaidia na kukupatia chochote, na ulikuwa na watu waliokuzunguka ambao uliwapa kazi na japo kidogo cha kuwasaidia. Kisha, ghafla hali inabadilika, na unakuta huna chochote cha maana. Mission za mjini zinakata, huonekani tena na unapauka. Mahitaji ya msingi yanaonekana kuwa anasa, na tabia za majungu zinakurudia. Unashindwa kujituma kutafuta, badala yake unatafuta njia za kupoteza muda. Hali hii huwa inatisha na kuchanganya sana.

Ninapokuwa mjini na kukutana na kaka zangu na watu mbalimbali kutoka hapa kwetu, hasa wale ambao miaka iliyopita walionekana wamefanikiwa au walikuwa njiani kufanikiwa, na sasa wamechoka. Uzee umeanza kuwaingia, na ngozi zao hazionekani vizuri. Wamechagua kufanya kazi ndogo ndogo kama bodaboda na mara nyingi wananiomba pesa. Niseme ukweli, nafsi yangu hujaa huzuni na hofu ninapowaona. Huwa najiuliza, wao walikosea wapi na mimi nina nini cha maana ambacho kinaweza kuwa ngao na uhakika wa maisha yangu?

Nikiwa kanisani, nimejikuta nikisali, nikimwomba Mwenyezi Mungu mwingi wa upendo anibariki siku zangu, aniondolee siku za mateso, aniepushe na mikosi, laana, na mabalaa. Naendelea kujiuliza, je, nini nilichonacho cha kipekee ambacho kinaweza kunipa uhakika wa maisha? Wewe unafanya nini ili usitoke nje ya mstari wa maisha na kuhakikisha maisha yako yanaendelea kunawiri, hata zitakapofika siku za uzee wako uwe mtu mwenye furaha?
 
Back
Top Bottom