Mogambi
JF-Expert Member
- May 25, 2012
- 209
- 356
Nawasalimu kwa jina la jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Ni matumaini yangu mu-bukheri wa afya.
Mara baada ya salaam hiyo naomba niingie kwenye hoja yangu moja kwa moja. Awali ya yote, mada yangu inajikita katika kuhamasisha uwajibikaji na uzalendo wa kitaifa.
Ni kitu ambacho kwa sasa kinachukuliwa kama jambo la kawaida na KIGEZO muhimu mahali pa Kazi, kuona kwamba wale wanaostahili na wenye sifa za kupata cheo, ni wale watu ambao hata kama hawana sifa za kiweredi, basi ni watiifu sana kwa wakuu wao kazini. Hapa, nisinukuliwe kwamba nahamasisha watu kutowatii viongozi wao. Hapana, utii ni sifa njema katika jamii tena sifa ya kupigiwa mfano.
Lakini hapa, nazungumzia wale watu ambao huonekana kuwa watii kwa wakubwa wao kwa UNAFIKI, wakitumia ile kauli ya mtumikie kafiri uupate ujira wako kama motisha ya kujipendekeza, kujipatia cheo cha ushushushu kwa ajili ya bosi na kutoa ripoti ambazo kwa namna moja au nyingine, zinaathiri maamuzi ya kiongozi mkuu, lengo lao wapate upendeleo, au cheo cha kimadaraka chenye kunukia fedha.
Ni wazi kwamba mahali pengi pa kazi, tunao watu hao ambao mara nyingi huonekana wema, watu wanaojitolea hata muda wao bure almradi wafanikishe lengo lao, huku wakijifanya kuwa wanasukuma agenda ya kiongozi mkuu. Na kwa vile viongozi wao wanakuwa wamepofushwa na zile tabia bandia wanazowaonesha, watu hawa hupewa nafasi kubwa ya kushawishi maamuzi ambayo huathiri mwelekeo wa taasisi kwa namna ambayo wao hunufaika. Tabia hii, kwa ujumla inaitwa UNAFIKI.
Wanafiki hukokotoa vema hesabu zao. Si rahisi kubaini njama zao kama kiongozi hana utashi na uelewa wa saikolojia ya watu aina hii. Ni watu ambao wako tayari kutangaza kwamba wanaamini katika dhana ambayo ipo tofauti kabisa/kinyume na mtazamo wao halisi, ili tu wamfanye kiongozi awe na imani kuwa wako pamoja.
Watu hawa, ni kama panya wanaong'ata na kupuliza. Huwezi kujua kama wanakutafuna hadi pale wanapokuwa wamemaliza agenda yao, na au wanajua wamekumudu, na hapo ndipo rangi zao halisi huonekana. Hao, husimama kidede kutoa siri na vyanzo vya madhaifu yako kama vidhibiti vya kukuangamiza bila soni, wakikutazama machopima bila kutahayari.
Miaka ya karibuni tumeshuhudia aina hii ya watu ikijitokeza hadharani bila kificho, na hata baada ya unafiki wao kuonekana wazi, tulio wengi tumezidi kuwafuata na kuwapa heko, na wamemudu hata kuhalalisha UNAFIKI kama njia mbinu muhimu ya kuishi (Necessary survival tactics).
Mwandishi Robert Greene, katika kitabu chake 'The 48 Laws of Power' amethubutu hata kuandika mbinu nyingi za kuutumia UNAFIKI ili kufikia malengo kwa mwanasiasa au mtaka cheo mahali pa kazi, na sasa kuna watu wengi wanadhani kwamba hiyo ni njia sahihi ya maisha. Hebu chukulia mfano viongozi wetu katika awamu ya tano iliyokuwa ikiongozwa na hayati Rais John Pombe Joseph Magufuli.
Wengi tulishuhudia mapambio yaliyokuwa yakiimbwa na viongozi hao, Ili tu kujihakikishia kuwa wanabaki madarakani kwa kuwa upande wa hayati Rais. Watu hawa, huenda walikuwa na mchango mkubwa sana katika maamuzi yaliyokuwa yanapitishwa katika awamu hiyo, yawe mazuri au mabaya.
Ajabu, na hili linashangaza sana kwamba, mara baada ya kupata kiongozi mpya mama Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, awamu ya sita, tumeshuhudia pambio mpya ambazo zinaimbwa na watu wale wale na ukichunguza kwa makini, zinalenga kuponda aliyepita na kumsifia aliyepo. Unafika sehemu unajiuliza, sio hawa hawa waliokuwa mstari wa mbele kusifia wanayoyakosoa na kuyapondaponda leo?
Watu hawa wasioona haya, wamekuwa vikwazo vya nchi/ taasisi kupiga hatua kwa sababu michango yao halisi hawaitoi kwa kuhofia kwamba huenda wakapoteza nafasi zao madarakani, na hivyo wamekuwa ni watu wa 'ndio mkubwa' hata pale wanapoamini maamuzi yanayochukuliwa si sawa.
Aina hii ya watu, tumekuwa tukishuhudia ikipewa nafasi kubwa na kupandishwa vyeo vikubwa vikubwa kwa sababu tu, wanaonekana vipenzi vya kiongozi mkuu mahali pa kazi, na mara nyingi upenzi huo ukitokana na sifa nyingine ya watu hawa, sifa ya kufitinisha wale wanaoonekana kuwa na Mawazo tofauti na kiongozi mkuu, hata kama yangelikuwa mawazo bora ya kujenga.
Katika muktadha huo, nchi/taasisi inakuwa inaendeshwa kwa fikra na utashi wa mtu mmoja. Hali ambayo inapelekea maamuzi yenye mrengo wautakao wao, ambayo yanakuwa hayana tija na ni mzigo kwa taasisi na hata nchi.
Kama hali hii ya UNAFIKI, hali ya kukosa uzalendo kwanza, ambayo hata baba wa taifa hayati Mwl J K Nyerere aliikemea katika hotuba zake, na yeye mwenyewe akionesha kukosoa pale alipoona inafaa, ikiachiwa kuendelea, taifa letu litakuwa taifa lisilokuwa na dira wala mwelekeo sahihi, tukiyumbishwa na masuala yanayotia ukakasi, ambayo yanayumbisha taifa kwa maslahi ya watu wanafiki.
Huenda ni mfumo wetu wa uongozi unaolea tabia hizi mbaya. Tabia ambazo si tu zinasalia kwa viongozi, bali zinashuka hata huku chini kwa raia wa kawaida. Kuna kipindi inafikia, mtu akipata ajira kwenye taasisi ya serikali asipofanya ubadhirifu wa mali za umma, jamii inamuona mtu wa ajabu.
Jamii, imefikia sehemu imeaminishwa kwamba serikali ikileta mradi kwa mfano kijijini, basi mtendaji wa kijiji, asipoiba saruji, na kununua vifaa duni na kulipua kazi, Ili tu abakishe fedha na baadaye aonekane amepiga hela ya kujenga jengo lake zuri au kunua gari, basi mtu huyo hutafsiriwa kama mpumbavu wa kiwango cha SGR.
Utasikia wanandugu wakimsimanga, 'hizo hela ni za bibi yako unavyozionea uchungu? Huoni mtoto wa fulani amesimamia mradi kama huo na amejenga kwa wazazi wake? Huo ujinga wako utakufa maskini, na bado wenzako watazipiga ubebe lawama au ufungwe wewe' na hapo utasikia pia wakisisitiza, 'amka wewe, acha uzoba. Usipotoboa kwa mradi huu, utakufa maskini.'
Hapo ndipo tumefikia kama jamii kwa kulea tabia ya UNAFIKI, unaolenga kujinufaisha binafsi.
Huenda, wewe pia ukaona kwamba ni jambo sawa, au ukasema potelea pote, na labda ukaenda mbele zaidi na kudai, kwa nini ufe maskini, au udumu kwenye hali duni wakati cha kufanya ni kujependekeza, kujikomba na kurombeza umbeya tu kwa boss, na uka-wini cheo, na kupata fursa?
Ajabu ni kuwa, wengi wetu tunahofia kufa maskini, lakini nikuulize ndugu yangu, ulisikia nani kafa tajiri? Wote maskini kwa matajiri hufa wakiwa maskini. Hawana mamlaka na mali yao waliyoyasaka kwa bidii na hata wengine kwa hila. Maamuzi ya mali hayo, yanabaki kwa walioachwa hata kama angeziandikia wosia wa namna gani zitumike. Mhubiri mmoja zamani, alihitimisha vema suala hilo, aliposema 'Ni ubatili na kujilisha upepo tu'
Lakini, hebu jiulize, pale mwanao kipenzi anapoumwa na hawezi pata matibabu kwa sababu kuna mnafiki mmoja amejitia mjanja na kupiga hela za dawa hospitalini, na anasikilizwa na mkubwa kuliko yanavyosikilizwa malalamiko yenu. Au, fikiria, mnaingizwa kwenye sera ambayo labda itapelekea watu wengi kupoteza uhai, au itakayohamasisha upotevu wa maadili kwa vile tu, kwa kupenda madaraka na vyeo, kuna mnafiki mmoja ameshawishiwa mshiko ahakikishe ajenda ya mtu mbaya huko nje ya mipaka ya nchi yetu, anapata urahisi wa kuingiza agenda yake nchini, labda ni madawa ya kulevya, na atakeyeathirika ni mwanao umpendaye!
Kiujumla, tabia ya UNAFIKI si tabia ya kukumbatiwa kwa sababu, faida zake ni kwa mnafiki mwenyewe, lakini hasara zake zinaangamiza taifa kwa ujumla.
'Haki huinua taifa, Bali dhambi ni Aibu ya watu wote' Mithali 14:34

Upvote
4