Unafikiri kwanini umeumbwa uishi, lakini badae unatakiwa ufe?

Unafikiri kwanini umeumbwa uishi, lakini badae unatakiwa ufe?

Just talker

Member
Joined
Jan 6, 2021
Posts
50
Reaction score
63
8117DC02-77F6-48E8-9FCB-FECB469729E3.jpeg

Unafikiri kwanini umeumbwa uishi, lakini badae unatakiwa ufe. Yaani umezaliwa unaishi lakini piga ua pamoja na mali zako badae unatakiwa ufe. KWANINI ???? Ni KWANINI..... wew haujiulizi sababu.

Mimi nakataa kuwa tumeumbwa duniani ili kumtukuza mungu na kumuabudu, kwasababu mungu hana kitu anashindwa hadi kutuleta sisi atutegemee au tumsaidie.

Kama unakubaliana na Mimi kuwa kifo ni lazima kwa kila mtu kuwa atakufa, utakubaliana na Mimi pia dawa za magonjwa huwa ni mbwembwe tu lakini huwa hazikizuii kifo. Ni kweli kuwa labda dalili ya kifo ni ugonjwa ndiyo maana tunahitaji tiba ili tuitoe hiyo dalili sio ili tusife ni ili tupone, kwasababu sio kila asiye pona anakufa ndiyo maana wapo wagonjwa hadi wa miaka 20 hawajapona na hawafi. Kama dawa zingezuia kifo basi walio zigundua wasinge kufa. Hebu ngoja Tuachane na habari za dawa tuendelee na mada yangu.

Unahisi kwanini mungu anaamua kutuleta duniani, wengine wanafika tu duniani nakufa hata pasipo kuiona dunia.

mfano;
watu wengine huzaliwa nakufa papo hapo, KWANINI sasa si bora hata mimba isinge ingia kuliko mama mtoto kukaa na ujauzito miezi Tisa halafu baada ya muda wa kujifungua kufika mtoto anakufa KWANINI.

Kwanini unatakiwa badae ufe, kwanini tu usingekuwepo kuliko uje duniani badae ufe halafu watu uwaumize, kulikuwa na haja gani ya wewe kuzaliwa.

Kuna sababu kubwa katikati ya maisha yetu. Yaani kama kuna kuzaliwa na kufa sasa kati kati ya kuzaliwa na kufa kuna sababu ambayo ndiyo naiulizia. KWANINI upo duniani na baadae unatakiwa kufa. Lazima kuna sababu, ndiyo kuna sababu KUNA SABABU kwanini.

Haya ndiyo majibu yangu ya swali hili. Huenda sio majibu sahihi kwa upande wako ila kwangu ndiyo nayo yaamini.

Sisi ni malaika wa mbinguni. Wengi wetu ni malaika waasi ambao tumeletwa duniani ili kubadilika, na kila mtu anamuda wake alio pewa wa kubadilika na pindi muda unapoisha ndio unatakiwa kufa kisha uende unakositahili.

ndiyo maana unaambiwa kanisani na msikitini kuwa usipo tenda dhambi ukifa unaenda mbinguni. Viongozi wa dini ni baadhi ya malaika wasio waasi, achana na viongozi fake wenye lengo baya na mungu yaani wauongo. Sasa hao viongozi ambao sio waasi wamechangamywa na wengine malaika sisi wadhambi kwa lengo la kutupa mafunzo ya kutubadilisha ili tunapo fuzu turudi kwetu mbinguni. Ukipuuza masuala ya mungu hadi muda wako ukafika wa kuondoka duniani basi utaungana na wenzako wadhambi walio goma kumkubali mungu.

Unatakiwa ujiulize kwanini shetani aasi mbinguni kisha aletwe duniani sehemu wanapo ishi watu wake mungu na viumbe vya mungu yaani sisi pamoja na wanyama wote alio waumba mungu, kwani mungu hatupendi anatuchukia?!! Hapana hatuchukii sasa KWANINI amulete mtu mbaya kwetu Au kwani unafikiri anashindwa kumuangamiza? Ila na yeye ni malaika wake ndiyo maana akaletwa dunia hii tuliyopo sisi malaika wenzake.

Kwahiyo Lazima uelewe sio shetani tu muasi hata sisi. Na lengo lake ni wote tubadilike, ndiyo maana vitabu vya mungu vinasema wadhambi watachomwa moto, vinasema pia sisi ni wadhambi. Lakini bado tunayo nafasi tumuombe mungu atusamehe.

Naamini sehemu yenye idadi kubwa ya watu kuishi ni kwenye ufalme wa mungu yaani mbinguni, ambako ukitenda dhambi utashushwa duniani lengo uje ukae na wenzako wadhambi walio shushwa ili kama utabadilika urudi tena nyumbani yaani mbinguni. Kwamaana nyingine Mimi binafsi naamini nyumbani kwetu ni mbinguni huku tupo mafunzoni tukishinda vile ipasavyo tutarudi kwetu mbinguni.

Swali? Kama umeamini kama ninavyo amini Mimi kama ulivyo nisikiliza.

Umekubali kubadilika?, umeshabadilika?

Swali kama unajibu lako je? KWANINI UNAISHI HALAFU BADAE UNATAKIWA UFE.

Asante; nifollow Instagram kwa jina la Donrugi 🙏🏻
 
mbona unajikanganya sasa?!!!

huko mwanzoni umesema huamini km tupo kwa ajili ya kumuabudu Mungu....umekataa!

baadae unasema sisi ni malaika tulioletwa kujirekebisha, huku ukitumia reference ya viongozi wa dini mara kadhaa (dalili ya kukubali ibada kama sijaelewa vibaya). weka sawa msimamo wako kwanza kabla ya yote!!!
 
Inaonekana mtoa mada una hoja fulani ambayo unapenda kuiwasilisha, ila tatizo linapokuja ni kwamba haufuati vigezo vya uandishi.
KUMBUKA: Kuhamisha kitu ulichonacho kichwani kwenda kwa mwingine, hasa kwa kutumia njia ya MAANDISHI ni jambo gumu mnoo. Hivyo tulia, jipange kisha uandike upya.
 
Hakika ana jambo kubwa sana ambalo hata mimi nimewahi kulifikiria siku nilipo lala njaa! (Sifanyi utani)

Sababu ya sisi kuzaliwa kuishi na kufa haijalishi umetenda dhambi wala haukatenda ni ipi?
Kisayansi inaweza kujibika kirahisi sana kuwa tunakufa kwa sababu nature haiihitaji species zilizozeeka na ili maisha yaendelee ni lazima kilichopo kife kije kingine.

Swali je na hivi vitoto au vijana wadogo kabisa nao ni species ambazo nature haizitaki?

OMG! 😢
 
Sina kodi ya nyumba, sina pesa ya pombe, sina Ada za watoto, CCM wameiba kura, yanga wamemfukuza kocha, Man u kamfunga City.... Kuna corona kila siku inanikosakosa nianz3 kuwaza ujinga huu tena? Njoo hapa Kigali tusungumse
 
mbona unajikanganya sasa?!!!

huko mwanzoni umesema huamini km tupo kwa ajili ya kumuabudu Mungu....umekataa!

baadae unasema sisi ni malaika tulioletwa kujirekebisha, huku ukitumia reference ya viongozi wa dini mara kadhaa (dalili ya kukubali ibada kama sijaelewa vibaya). weka sawa msimamo wako kwanza kabla ya yote!!!
Nimejikanyagaje sasa, tumekuja kubadilika sio kuabudu
 
mbona unajikanganya sasa?!!!

huko mwanzoni umesema huamini km tupo kwa ajili ya kumuabudu Mungu....umekataa!

baadae unasema sisi ni malaika tulioletwa kujirekebisha, huku ukitumia reference ya viongozi wa dini mara kadhaa (dalili ya kukubali ibada kama sijaelewa vibaya). weka sawa msimamo wako kwanza kabla ya yote!!!
Hata Mimi wakati nasoma niliona,, mleta mada anaamka usingizini huku anajifunika shuka,,
 
Hadith za kwamba Mungu anaabudiwa walizileta wayunani wa kale,wayahudi wakazikazia kwenye dogmas zao na kuzifrem kikatokea kitu kinaitwa dini wakawalisha RAIA zao kwa kuwajaza hofu,utiifu na unyenyekevu kwa huyo wanayemwamini ingawa yeye huyo Mungu hajishughulishi na wewe mbaka umnyenyekee na kumsujudu bila ya hivyo hajishughulishi na mtu yeyote!

maoni yangu tu .

Povu ruksaaa!
 
Hakika ana jambo kubwa sana ambalo hata mimi nimewahi kulifikiria siku nilipo lala njaa! (Sifanyi utani)

Sababu ya sisi kuzaliwa kuishi na kufa haijalishi umetenda dhambi wala haukatenda ni ipi?
Kisayansi inaweza kujibika kirahisi sana kuwa tunakufa kwa sababu nature haiihitaji species zilizozeeka na ili maisha yaendelee ni lazima kilichopo kife kije kingine.

Swali je na hivi vitoto au vijana wadogo kabisa nao ni species ambazo nature haizitaki?

OMG! [emoji22]
Upo sahihi kabisa mkuu. Maswali ni mengi sana ambayo yanahitaji muda ili kupata majibu, na ugumu unakuja pale tuu ambapo majibu ya maswali hayo yatajikita kwenye mtizamo na experience ya mtu husika. Hivyo ni nadra sana kupata majibu common, kwa sababu mazingira ni tofauti pia. Kwa mfano; wewe ukitizama UHAI kama muda ambao mwanadamu amepewa ili atengeneze maisha yake ya baadae/milele. Mwingine atachukulia kama ni jambo la KURITHISHANA(Like produce like) kama ilivyo kwa mimea, wadudu, ndege n.k Swali ni je!? Nao wapo ili wajirekebishe kama anavyodai mtoa mada??
 
Back
Top Bottom