Unafikiria ingekuwaje kama pasingekuwepo kitu chochote?

Unafikiria ingekuwaje kama pasingekuwepo kitu chochote?

KENZY

JF-Expert Member
Joined
Dec 27, 2015
Posts
32,529
Reaction score
76,691
Hakuna hewa, maji, mwanga, giza na kitu cha aina yoyote ile je, unafikiri pangekuwaje? Hali hii ya kutokuwepo chochote unadhani inawezekana?

Kama inawezekana, je inawezekanaje?

Wadau majibu tafadhali.

Karibuni
 
Hakuna hewa,maji,mwanga,giza na kitu cha aina yoyote ile je,unafikiri pangekuwaje..?
hali hii ya kutokuwepo chochote unadhani inawezekana..?
kama inawezekana,je inawezekanaje..?
wadau majibu tafadhali..
karibuni

Je unaongelea kwenye dunia hii au universe? Lakini unapoongelea mwanga duniani maana yake umehusisha Jua, na mwanga na giza umehusisha dunia kujizungusha katika muhimili wake. Jibu rahisi ni kwamba hali yawezekana kuwa kinyume na sasa au tofauti na sasa na sio kinyume na sasa ingawaje hakuna mtu wa kutoa empirical evidence kwani ata yeye hatakuwepo na sisi wote hatutakuwepo labda kama hali hii ya sasa itarudi tena na sisi tukiwa vilevile ikiwemo memory ya hali zote mbili - experimental and control time.

Halafu research ya hii kitu ni unethical kwani experiment ya kukosa hewa ni wewe kuzibwa wind pipe yako (mfumo wa hewa) au kunyimwa oxygen na matokeo yake ni kifo - hivyo ukiondoa hewa life tunayoijua haitakuwepo.

Halafu ukumbuke kwamba katika universe kuna dark energy na matter vitu ambavyo bado hatujavielewa bado; na kunauwezekano kuwa uelewa wetu sio sahihi kwa kiasi fulani. Hivyo nini kitatokea yaweza kuwa ngumu ku-predict.

Kwa kifupi science tayari inajaribu kutuambia hali itakauwa tofauti na very likely kinyume na sasa au tofauti na sasa mbali na kinyume na sasa.
 
Hakuna hewa,maji,mwanga,giza na kitu cha aina yoyote ile je,unafikiri pangekuwaje..?
hali hii ya kutokuwepo chochote unadhani inawezekana..?
kama inawezekana,je inawezekanaje..?
wadau majibu tafadhali..
karibuni
Usingeweza hata kuuliza hili swali.
 
Usingeweza hata kuuliza hili swali.
sidhani kama umenielewa.
unafikiri pangekuwaje kama pangekuwa hakuna kitu chochote..?
mtu akikuuliza mahala fulani pakoje si utamjibu kulingana na sehemu hiyo palivyo.
najua nisingeweza kuuliza ndio lkn pangekuaje..?
 
Ulishawahi kusikiliza kwa kuweka sikio kwenye mdomo wa chupa ya kuhifadhi chair??
 
sidhani kama umenielewa.
unafikiri pangekuwaje kama pangekuwa hakuna kitu chochote..?
mtu akikuuliza mahala fulani pakoje si utamjibu kulingana na sehemu hiyo palivyo.
najua nisingeweza kuuliza ndio lkn pangekuaje..?
me nadhani isingekua kitu maana hamna vitu na kusingekua na mtu awae yoyote wala kitu chochote
 
Hata swali hili lisingeulizwa, talking imaginal things, empty views
 
hebu niambie picha/muonekano wa kutokuwepo kwa kitu chochote ikoje...?

Hapo natamani kukwambia kwamba kama nitaweza kukwambia juu kisichokuwepo, basi ujue naweza pia kuiona kesho kwa kutumia urefu wa kimo changu...
 
me nadhani isingekua kitu maana hamna vitu na kusingekua na mtu awae yoyote wala kitu chochote
unaweza kuntel muonekano wa hali hiyo ya kutokuwepo kitu chochote..?
 
hebu niambie picha/muonekano wa kutokuwepo kwa kitu chochote ikoje...?

Picha ya wewe kutokuwepo ni kabla mimba yako haijatungwa na wewe kuzaliwa. Au kama una watoto weka hii picha kwa watoto wako. Mfano mwingine mzuri wa ku-perceive 'nothing' including yourself ni ukiwa umelala usiku au mchana na usiwe kwenye ndoto yaani ukiwa kwenye non rapid eye movement (deep sleep).
 
nisingefikili chochote maana natumai hata mie nisingekuwepo.. wala fikra za kuwaza ingekuaje zisinge kuwepo pia
 
Hakuna ajuwaye kwa maana hata sisi tusingekuwepo
Hili swali linakutaka ufikirie kama sasa tupo kuna haya yote mwanga,giza,hewa n.k je kama kusingekuwepo kitu chochote pangekuwaje..?
achana na habari kwamba usingekuwepo,ndio usingekuwepo lkn upo sasa.
 
Back
Top Bottom