Unahitaji D mbili kujua kwa nini tunafurahi kucheza ugenini Libya kwenye full house?

Unahitaji D mbili kujua kwa nini tunafurahi kucheza ugenini Libya kwenye full house?

SAYVILLE

JF-Expert Member
Joined
Mar 25, 2010
Posts
7,895
Reaction score
12,975
Kucheza ugenini uwanja ukiwa full house kama ilivyokuwa juzi kule Tripoli, Libya, kwanza ni exposure kubwa kwa wachezaji wa Simba ambao hawana experience ya kutosha kwenye mechi za kimataifa, hasa kucheza kwenye mazingira yasiyo rafiki kama yale. Kina Ahoua, Balua, Kagoma na wengine walikuwa wanabatizwa kwa moto.

Tuliache hilo. Unapokuwa na watazamaji 50,000 pale uwanjani, chukulia kila mtu pale ameacha wastani wa watu wawili nyumbani wanaojua ameenda kuiangalia Simba. Inamaanisha hapo tayari ni watu 150,000 wanaojua Simba inacheza leo na wengi wataifuatilia mechi kupitia vyanzo mbalimbali.

Hapo sijaongelea wale ambao hawana uhusiano wa moja kwa moja na wale waliopo uwanjani, weka makadirio yako unayotaka wewe. Hiyo ni fursa kubwa ya kujenga brand mioyoni na machoni mwa hao Walibya (hata kama walikuja kisharishari). Hata mechi ya marudiano ya Dar, wengi wa hawa watafuatilia mechi hiyo, fursa nyingine ya kusindika zaidi brand ya Simba mioyoni mwao.

Soma Pia: FT: Al Ahly Tripoli 0-0 Simba SC | CAF Confederation Cup | Tripoli International Stadium | 15/09/2024

Kesho ukisikia Simba ni moja ya timu zinazofuatiliwa zaidi, usianze fitna na roho mbaya, watu wamewekeza misingi ya jasho jingi inayowezesha hayo kutokea.
 
Back
Top Bottom