Lycaon pictus
JF-Expert Member
- Jan 31, 2021
- 9,189
- 16,128
Siki ni nini? Siki hutokana na pombe. Ili kutengeneza pombe fangasi hubadili sukari(Glucose) kuwa pombe(Ethanol). Sasa kuna bakteria wanaweza kuibadili hiyo ethanol kuwa asidi(Acetic acid), na hiyo ndiyo siki. Kiasili siki inatoka kwenye pombe. Kwa wakazi wa nyanda za juu kusini watakuwa wanafahamu ulanzi unaoitwa mkangafu. Ni ulanzi uliokaa muda mrefu na huwa mkali sana, wengi wanadhani kuwa ndiyo unalewesha sana. Si kweli, ulanzi ule pombe yake inakuwa imebadilika kuwa acetic acid. Unakuwa unakunywa maasidi yasiyolewesha.
Ukichukua pombe, kama wine na ukaiacha kwa muda mrefu utaona bakteria hawa wameanza kujijenga. Juu ya hiyo pombe hutengeneza utando mzito unaofanana na maini mabichi. Huo huwa mchanganyiko wa bakteria wa kutengeneza siki. unaitwa Mother of Vinegar. Hata juisi ukiiacha kwa muda mrefu utaona inatengeneza pombe na kisha kuunda huo utando baada ya bakteria kuanza kutengeneza siki.
Siki inatumika sana kwenye msosi. Ni kama limao au ndimu kwenye chakula. Pia kwa sababu ni asidi, inafaa sana kusafishia vitu. Inang'arisha sana. Pia wengine wameitumia kama dawa na pengine kutesea watu kama walivyofanya kwa Yesu. Wale waliomtesa walizamisha kitambaa kwenye siki na kumnyooshea anywe.
Mother of vinegar(Mama siki) akiwa ametolewa kwenye vinegar.