Unaijua CHUMAULETE?

Fabian the Jr

JF-Expert Member
Joined
Aug 4, 2012
Posts
756
Reaction score
751
Habari wakuu,
Nipo katika mchakato wa kufungua biashara mahali, lakini nikiwa katika mchakato huu kuna jamaa aliniambia, "aisee kuwa makini na chumaulete mtaa huu"

Nahtaji kujua yafuatayo,

Ni kweli chuma ulete ipo i mean inafanya kazi? Au ni story tu za mtaani? Kuna yeyote ambae ashawah kukutana nayo?

Ni kweli kabisa kwamba mtu anaweza akaja na buku, ukiichanganya kwenye droo yako yenye mil 50 zote zinapotea?

Je kama ni kweli, ni namna gani naweza kujiepusha na chumaulete.
 
Kweli au si kweli ni imani yako tu, ukiamini ni kweli inakuwa kweli na ukiamini si kweli basi inakuwa si kweli.
 
Kuna mambo mengine huwez kuyaamin mpaka yakutokee hata ukielezwa kias gan.....

Kama unaiman sehem unayoweka pesa zako hapo dukan weka ma kamkaa kidogo ila kama unaimam....

By ze way nenda katika nyumba ya ibada kwa iman yako sali sana
 
Acha hizo imani mkuu, kama una nia ya kufanya biashara fanya, huna nia piga chini, na c kuhoji vitu vya ajabu kama hivi!!
 
IPO Nina experience nayo ukishaona au kumjua mzee Fulani anahizo tabia basi hela yake usiichanganye iweke chini kisha ikanyange kwa mguu

Asubuhi ukiwa inafanya mahesabu ndo ruska kuichamganya na fedha nyengine ni hayo tu
 
Bado hakuna jibu sahihi...tumsubiri mshana
 
IPO Nina experience nayo ukishaona au kumjua mzee Fulani anahizo tabia basi hela yake usiichanganye iweke chini kisha ikanyange kwa mguu

Asubuhi ukiwa inafanya mahesabu ndo ruska kuichamganya na fedha nyengine ni hayo tu
[emoji12] [emoji12]
 
Mkuu hyo kitu ipo ni kama uchawi upo ila hauonekani ila fanya kazi na sala utayasikia kwa wenzio maana ulinzi wa muumba utakuwepo.
 
Hiyo ipo, kwani ni aina fulani ya "mazingaombwe" na dawa yake kubwa ni kumtegemea Mungu kwa kufanya maombi katika shughuli zako za biashara.

Hii inataka kufanana na kile kisa cha wachawi wa Firauni (Farao) na Nabii Musa------ Wale wachawi walipotuka kamba zao zikaonekana kwa watazamaji zimekuwa nyoka lakini hazikuwa nyoka kidhahiri bali ilikuwa ni mazingaombwe viini macho tu ndipo Mungu akamfunulia Nabii Musa atupe fimbo yake na maramoja hila za wale wachawi zikabainika kwa fimbo ya Musa kumeza wale nyoka bandia wa wachawi. Mazingaombwe hapa ni ile hali ya macho kudanganyika kutokuona uhalisia wa tukio na hii hali ndiyo inatumiwa na hao chuma ulete, wanatumia elimu hiyo kukuhadaa na unashindwa kutambua na wewe mwenyewe unatoa ela kumpatia bila kutambua hadi hapo baadaye unakujaona hela hakuna na kuanza kushangaa imekuaje.
 

Nimeipenda hii
 
Chuma ulete zipo za mitindo mingi tu, kuna ambao wanakuja na kipande tu cha karatasi ila wewe itaiona kama noti ya tsh 10,000/=, kwa hiyo hapa atakuwa amechukua bidhaa bure na chenji ya bure, pia kuna wengine wanachukua bidhaa bila ya kununua, yaani mchawi yule anapita ktk biashara yako anachagua chagua kisha hanunui anaacha, kumbe wakati ule anashika shika ndio anabeba bidhaa wewe hujui, na pia kuna wengine wanatumia mandondocha kuja kukusanya ushuru katika kila biashara ila wewe huwaoni, hizo ni baadhi tu ya njia wanazotumia. Ila ukiwasikiliza hao wakimbizi watakwambia hakuna kitu kama hicho
 
Haya mambo yapo,hata mimi nilikuwa mbishi sana lakini nilithibitisha mwenyewe na nikaweka kinga npaka leo mambo poa
 
Unapoweka pesa yako make sure Kama ni mkristo bible haikosi..pia sali nakumtumainia mwenyezi
 
Jambo muhimu kwa kila Muislamu ni kujikinga na mambo ya sihri na mashetani kwa kusoma badhi ya aya na Surah za Qur’ani na Adhkaar alizozifundisha Mtume Muhammad (Swalla Llaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam). Miongoni mwazo ni Suratul Faatihah, aya kumi za Suratil Baqarah (aya 1 – 5, 255 – 257 na 284 – 286), Suratul Kaafiruun, Suratul Ikhlaasw (mara 3), Suratul Falaq na Suratun Naas (mara tatu tatu) na Adhkaar ambazo kila mmoja anaweza kuzipata katika vitabu.
KAMA WEWE SIO MUISLAMU BASI WATAKUJA KUKUELEKEZA KWA MUJIBU WA UKRISTO MANA HAYA NI MASUALA YA KIIMANI NA KIROHO
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…