Unaikubuka Mbeya City ya mwaka 2013/2014?

Matanga

JF-Expert Member
Joined
Nov 13, 2019
Posts
2,281
Reaction score
3,976
Mahali hapa si salama kwako ila ndio sehemu tunayoishi sisi, ndani ya dunia hii kuna sehemu huwezi kugeuka mara mbili kuitazama sehemu kama ukanda wa gaza palestina, ni moja ya maeneo duniani ambayo roho yako inakuwa haina uhakika wa kuwa ndani ya mwili wako katika sekunde moja ijayo, roho yako inatazama kuzimu kuliko ulimwenguni, ila kuna wanadamu wanaishi hapo na maisha yanaendelea kama kawaida.

Ndani ya soka kuna maisha haya pia, kuondoka na ushindi kwa timu pinzani kwa baadhi ya viwanja si kazi nyepesi, uwanja kama wa Anfield, Nou Camp ni adhabu tosha kwanza kucheza hapo unapigiwa mpira mwingi huku kelele za mashabiki wao zikikulevya, Tanzania msimu wa mwaka 2013/14 klabu ya Mbeya city iliufanya uwanja wa sokoine kuwa kama ukanda wa gaza, kushinda pale ilikua kama kujaribu kujipiga risasi ukiamini utapona haikua kazi rahisi, ingawa iliwezekana.

Wakijulikana kama wabishi wa Mbeya waligeuza Tanzania kuwa ya zambarau pale walipokuwa wakicheza, kila timu iliyocheza na Mbeya city haikutamani kucheza nao tena, wakiwa na wachezaji waliosheheni upambanaji Deus Kaseke, Saady Kipanga huku wakicheza kitimu zaidi bila kuchoka kila baada ya dakika 90 kuwatazama Mbeya city ilikua zawadi tosha kufurahia maisha.

Shamra shamra waliyokuwa nayo mashabiki wa Mbeya city ilikua kubwa walisafiri na timu kila sehemu, hawa ndio waliomba mechi yao dhidi ya Azam ichezwe uwanja wa taifa badala ya azam complex kuhofia uwanja kutotosha, walikua sahihi uwanja ulifurika ikapigwa shoo ya kiutu uzima kwa wauza juisi, mechi ikamalizika kwa sare ya mabao matatu kwa matatu, hatrick ya ticha Mwagane yeya ikazungumza na taifa kwa muda.

Wakitoka kupanga daraja tu msimu uliopita Mbeya city walikuwa moto uliokamilika, Anthony Matogolo kiungo fundi ndani ya timu alikua kama laini ndani ya simu, bila yenyewe simu haina kazi, pasi zake mahiri, ukabaji wake wa kitaalamu ilikua ni kama kupiga simu na kuongea bila kukatwa salio, walikuwa smart sana kiuchezaji hawa jamaa.

Wakamaliza ligi wakiwa nafasi ya tatu, wakifunga zaidi ya goli 32, lakini muda mwingi walikuwa wakifukuzana na Azam, Yanga katika mbio za ubingwa wa msimu huo ulioshuhudia Azam wakiwa mabingwa kwa mara ya kwanza katika historia yao katika ligi kuu Tanzania bara.

Baada ya msimu kumalizika mambo mengi yalibadirika ndani ya timu, wachezaji tegemeo waliondoka ndani ya timu, maisha yao yakajaa hofu sana, hata wale mashabiki waliovutiwa na timu hii wakaanza kukosa imani, mapenzi yao taratibu yakaanza mbawa, hata kwa sisi wapenzi wa soka ilituumiza sana.

Kwa sasa wamebaki kama washiriki unaona wanapambana kubakia ligi tu hawana tofauti na timu nyingine za mikoani, mbio za ubingwa haziwahusu tena, ukikutana nao waambie wafanye kurudia yale waliyoyafanya msimu wa 2013/14, kwenye maisha yote yanawezekana Mbeya pamepoa sana siku hizi wakoma kumwanya.

MIWANI YANGU



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nimemkumbuka Saady Kipanga hatareeeee vijana walikuwa moto moto,siasa ikaja kuwamaliza vijana wale
 
Mchawi mkuu wa Mbeya city hadi sasa ni Mwambusi na hakika binafsi namchukia maana aliutumia timu kufaidika nayo na sasa alioshirikiana nao kuiua mbeya city Yanga nao walishamtema.



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mwaka huo nilikua Mbeya pale Sae. Kituoni kabisa kulikua na tawi lao, jioni nilikua naenda pale kupiga stori. Siku hiyo nikakuta stori mashabiki wanalalamika kwamba Sugu hajawapa hela aliyowaahidi siku alipoenda kuwasalimia na siku hizi anawaruka.

Mimi nikawaambia kwanini msimuombe Sugu afanye mpango mpate mdhamini? Mtamuomba pesa mpaka lini? Mmoja aakajibu 'Yeye ni mbunge anatakiwa ailee timu' yaani Mbeya ilikua na mentality sawa na timu yangu ya mtaani niliyochezea ambayo tuliamini mwenyekiti wa serikali ya mtaa ni lazima kutulea.
Nikajua tu ukata ukishika hatamu hapa plus mipango hakuna hawa yatawakumba ya Moro United.

Mbeya City ni kama Southampton, walishain msimu uliofuata kila mtu akaenda pale kuchagua aliyemtaka, na kwakua timu za Tz hazina vijana wa akiba basi kifo kikawa kimekaribishwa.
 
Hilo ndiyo tatizo kubwa la timu zetu tumezidi kuwa tegemezi jamani

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…