Unaishauri nini Simba?!

1. Tafuteni match analyst mumpe ajira haraka awasidie kuwasoma maadui kwani inaonekana benchi la ufundi la Simba lina uwezo mdogo sana katika eneo hili.
2. Undeni scouting team ya watu watano mpaka kumi iwe based Dsm. Ambayo ndani yake wawepo wachezaji wa zamani, makocha wa zamani, waandishi wa habari n.k. Halafu tafuteni mashabiki wa Simba nchi nzima wenye ufahamu na mpira. Then waunganisheni na scouting team iliyopo Dsm. Tafuteni wapenzi wa Simba wanaoishi nje ya Tanzania hasa Ghana, Cameroon, Nigeria huko kuna wachezaji wa kiwango cha juu lakini bei zao rahisi kwani wao wanatafuta tu platform ya kutokea kimataifa. Pia na wao waunganisheni na scouting team. Kwa namna hii ikitokea mchezaji mzuri mkoani au nje ya nchi wanaweza kwenda hata watu watatu wa scouting team kumfuatilia bila ya mchezaji kujua. Hii itapunguza gharama ya usajili na uwezekano wa kupata wachezaji wenye viwango vikubwa bila kupigana vikumbo na vigogo wa Afrika.
3.Boresheni timu za vijana na muwape mikataba ya muda mrefu. Hii itaiwezesha Simba kupandisha wachezaji kwenye timu ya wakubwa watu ambao watakuwa na uchungu na timu yao pia timu itakuwa na uwezo wa kuuza vijana kwenye timu nyingine na kuingiza mapato kwenye klabu.
4.Msemaji wa timu afungwe gavana. Wakati mwingine inakera sana unapomuona anakejeli Yanga kama vile Mungu ni wa Simba tu. Wakati mwingine kwenye maisha ya kawaida tunajitafutia laana wenyewe kwa kuwakejeli wenzetu kwa sababu sisi tunajiona kuwa tumepata na Mungu ndio huja hapo kujidhihirisha kuwa yupo kwa wote hata wale tunaowaona kuwa wamekosa. Je tumejaribu kujiuliza ilikuwaje fowadi ya Simba ambayo inaaminika kuwa ndio kali kuliko zote kwenye ligi ya bongo ilikosa magoli ya wazi namna ile zaidi ya manne ndani ya hatua 6 kutoka kwenye goli? Je fowadi hiyo hiyo ilishindwaje kupata hata goli moja la kona licha ya kupata kona zaidi ya kumi? Jibu tulikosa bahati. Lakini inaaminika kuwa bahati mara nyingi huambatana na matendo yetu tunayowatendea wengine. Ndio maana leo kikosi cha Yanga chenye thamani ya chini kulinganisha na Simba kipo raundi ya pili wakati Simba wanarudi kucheza ligi.
5.Viongozi nao wajitathamini. Je walimpatia kocha wachezaji aliowahitaji wakati wa usajili? Je waliwaacha wachezaji kwenye usajili wachezaji alioshauri kocha waachwe nje ya Zana Kolibaly (hili lilikuwa garasa la kocha kulikuwa hakuna mjadala kuachwa kwake)? Kama viongozi walitimiza matakwa ya kocha basi wakulaumiwa ni kocha lakini kama hawakutimiza matakwa ya kocha basi walaumiwe viongozi kwa matokeo.

Lakini mwisho wa siku mpira ndio ulivyo na siku hazigandi na maisha lazima yaendelee. Simba sasa ijipange kwa ligi na ijue kuwa ligi ya mwaka huu si ya mchezo mchezo hata kidogo.
 
Simba wamtimue Kocha Uchebe. Kashindwa kufikia malengo, Kamtia hasara Mhindi, Kasajili Wabrazil na ameshindwa kuwatumia.
 
Asee umeongea kitu simpo lkn kikubwa,binafsi nimekuelewa
 

Big brain,thank you!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…