Huyu jamaa hapa chini naye ameweka ulabu kwenye chupa ya mtoto ya kunyonyea maziwa. Huyo mtoto naye ana chupa ya bia, ila sijui kilichopo ndani yake (maybe yamo maziwa !!). Hebu waangalie wote na ulinganishe. Sasa tusemaje, tuhoji hivyo "vyupa" walivyoshika au vimiminika vilivyomo ndani yake?
Kwa mtindo huu Serikali itabidi iongeze kiwanda kingine cha Bia,
Naamini Afande Kova au IGP Mwema wana mahudhurio mazuri hapa jamvini ingawa kwa kificho. Picha wanaziona, wanachotakiwa ni kumshughulikia huyu Mama kwa mujibu wa sheria.
Unamzungumzia mama gani? Huyo aliyeshika chupa za bia? kama ni huyo mimi sioni kosa lake kisheria.
Au unamhusisha na mtoto anayekata kilaji? kama ni hivyo, basi ni vema ukatueleza kinagaubaga kuwa huyo mama ana uhusianao na tendo la mtoto kunywa bia kwa maana picha hazionyeshi uhusiano huo
Mkuu Indume Yene,si rahisi kwa polisi au vyombo vya umma kuingilia suala ambalo mtoto anaruhusiwa kunywa .Panapotokea fujo hapo dola ndo pake.
Hili ni tatizo la kijamii zaidi na ni kielelezo cha kuporomoka kwa maadili dhahiri ya kiafrika.
Nafikiri wale wanaomzunguka mtoto akinywa nao wanajukumu la kufanya, hivi wtu hawa wanapomwona mtoto kinda kabisa akinywa wanasemaje, aaah poa tu!
Basi hata polisi wakija hapo hakuna mashahidi.
really? kuna watoto 4 wamelipuwa bomu kule moshi, 19 wamekufa Tabora...
Avatar yako utata yaweekana mama mtoto ni meber humu kaona avatar yako kashaiwshika kumpa mtoto wake pombe tena kamuanzishia vibaya na SAFARIuchagani hata katoto kadogo kananyeshwa mbege!!!!
Jamani hebu tuuache huu Utamaduni wa Kuilaumu serikali kwa kila kitu hata kwa vitu vcisivyo na msingi. sasa hapo serikali inahusika nini? au unataka siziwekwe mtandaoni kwa kuwa zina sifa mbaya wakati ndio ukweli halisi?
watu wanamatatizo yao na raha zao na kila mmoja ana life style yake mimi sioni cha ajabu hapo.
Labda uulize Wazazi wa sasa tunaenda wapi ktk malezi ya watoto wetu? sio serikali jamani!
Mkuu Indume, nakubaliana kabisa na wewe, na pengine wale watu wazima wote walio karibu na watoto hao wakati wakinywa inabidi wachukuliwe hatua vilevile.Hili jambo lasikitisha sana.Sina hakika kama kuna sheria inayomlinda mtoto dhidi ya ulevi wa aina hii. Kuna tofauti gani mtu anapomuingilia mtoto kimapenzi na kumpa mtoto kilevi? Kama hakuna sheria ya namna hii serikali kupitia wabunge wetu wanatakiwa kufikiria mara tatu tatu.
Kumlawiti au kumuingilia mtoto kimapenzi adhabu yake inatakiwa ilingane na hii ya kunywesha watoto vilevi kabla hata hawajafikisha miaka 18.
Waungwana nafikiri kinachohitajika hasa ni elimu kwa wazazi wa aina hiyo juu ya swala zima la malezi na wajibu wao kwa watoto tunaotegemea wawe taifa la kosho. Magereza yamejaa kiasi huduma kwa hao waliomo ni finyu,nafasi zilizopo zisubiri mafisadi waliopo on line.
Kuna ka imani ka ki-albinoalbino hivi kwamba watoto wakionja pombe katika umri huo ukubwani hazitawasumbua!
Pili, mbona mambo haya yanafanyika tangu zamani kwenye pombe za kienyeji? Au wengi wenu humu mmezaliwa WODINI?