Unaishi kwa Mshahara Peke Yake?

mkonowapaka

JF-Expert Member
Joined
Feb 19, 2010
Posts
1,492
Reaction score
768
Happy workers day jana wana JF

naamini wengi wetu hapa tumeajiriwa kwenye ofisi mbalimbali na wachache wamejiajiri.........ni sawa!

tukirudi kwenye uhalisia wa maisha ya kila siku;pamoja na garama za maisha kuendelea kupaa bila matumaini ya kuongezeka mishahara........still wafanyakazi walio wengi wana mazingira yasiyo rasmi hasa kwenye vipato zaidi ya mishahara.


Tuanzie chini kwamba Je mishahara tunayopokea inatutosha?na kama haitoshi..tunaishije..!

Je wewe mshahara wako halali unakutosha?unaishi kwa mshahara pekee?....huna muda wa ziada kufanya biashara nyingine..so kipato chako kinaongezekaje..ufisadi utakua unaanzia hapa..tujadili
 
kwa kweli watanzania nawapigia salute kwa kujua kupanga bajeti,unakuta mtu anapokea laki sita tu ana mke na watoto wanakwenda shule vizuri kabisa,na wanakula na kuvaa vizuri na mahitaji mengine na housegirl juu wanae na wengine wanapata ya kusave kidogo ya kujenga taratibu.Kuna kazi nyingine zina mianya ya marupurupu ambapo hapa ufisadi unaweza kuwepo ila kazi nyingine mishahara ni midogo na mianya ya marupurupu hakuna lakini watu wanaishi,ni kwa kujua tu kupangilia vizuri kidogo mtu apatacho.
 
inategemea how ambitious you are...hakuna kitu kama mshahara unatosha..kuna watu wanalipwa million 10 kwa mwezi lakini bado anahangaika huku na kule kutafuta madili mengine kwa sababu aim yake ya maisha iko juu anataka zaidi na zaidi...watu wengi siku hizi hawaishi na mishahara yao pekee hata kama wanalipwa million ngapi...
 
Kwa kweli hali halisi ya maisha ni ngumu sana, mshahara hautoshi, ila sasa wengine tunaokolewa na rasilimali tulizoachiwa na wazazi wetu, tumeziendeleza ndiyo maana tunafaidi na kuona mshahara wa laki tano,sita hadi sana na nusu kama ni unatosha kuendesha maisha lakini hakuna kitu kabisa ni sawa na bure.
 
So far inanitosha, no complains.
 
mie nina kibuzi,kinatop up matumizi madogo madogo kama vocha....:embarrassed1::tape:
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…