SoC01 Unajikuta kifungoni katika harakati za kutafuta uhuru

SoC01 Unajikuta kifungoni katika harakati za kutafuta uhuru

Stories of Change - 2021 Competition

msakhara

JF-Expert Member
Joined
May 26, 2019
Posts
277
Reaction score
381
Tumeumbwa kukua, kupiga hatua, na kuendelea kimwili, kiakili,kiuchumi na kijamii. Binadamu yeyote huumizwa na udumavu katika sekta yoyote kati ya hizo. Tunatamani sana jana na leo ziwe na utofauti chanya. Tunatamani baada ya muda tuwe huru, na uhakika wa kujihudumia sisi na tuwapendao

Je, tunaitofautishaje jana yetu na leo?,
Hapo kila mtu atakuja na jibu tofauti na ndipo upekee wa watuhuonekana.
Kunawatu wanakua na mikakati chanya na hasi kwenye hili, harali na haramu,.
Kuna watu na taasisi hutumia swali na utofauti wa majibu ya swali hilo kama fursa kiuchumi!
Mfano mzuri ni taasisi zinazokopesha watu mf. Mabenki.

Katika kuhangaika, kuitofautisha jana na leo na kukwepa maumivu ya udumavu na kukosa uhuru, watu wengi wamejikuta wakiingia kwenye meno ya taasisi hizi bila ya kujua namna gani watanufaika wao.
Watu wengi hasa wafanyakazi wa serikali na mashirika binafsi wanaishi kwenye minyororo ya madeni na maisha ya tabu sana kiuchumi baada ya kukopa kwa sababu zisizosahihi.
Badala ya kupata ule uhuru ama ukuaji waliotegemea, unakuta wamejifunga wenyewe!!

Kukopa ni jambo 'neutral' (halina uzuri wala ubaya), ila kwanini unakopa? Ndiyo inaweza leta uzuri ama ubaya wa hicho kitendo.

Kabla hujachukua mkopo jiulize;

-Je unataka kuutumia kufanya nini?

Haushauliwi kutumia kwenye vitu visivyoweza kurudisha pesa(liabilities) , au kwenye biashara inayoanza(startup).
Usikope kwa kufwata mkumbo 'niwe na usafiri kama boss',. Utakayeumia ni wewe na wa kwenu!
Kunawatu hukopa kwa lengo zuri ila hatimaye hushituka hela imeishia bar na kuhonga!! Mateso yanafwata,
Na kunawatu hukopa kwa lengo zuri ila bahati haikuwa upande wao(hii ni nje ya uwezo wetu)!


-Je unaelimu sahihi ya mkopo na masharti, riba yake?
Hii itakusaidia kujitathmini je huo mkopo kwako ni fursa au ni kifungo kwako. Itakusaidia kujua ni taasisi ipi ni nzuri kuliko nyingine kwa kutoa mkopo wa kiasi hicho na uwezekano wa wewe kulimaliza deni ndani ya muda muafaka na kukuepusha na fedheha kama kuuziwa nyumba n.k,

Je, baada ya kukopa, makato yataathiri kiasi gani kipato chako?

Hii itakuepusha kuwatesa watu wasio na hatia(watoto) na kujitesa wewe kama kipato kitaathirika sana, hakikisha unabakiwa na kiasi kinachotosha kujikimu kuishi kibinaadamu na dharula.
Kuna watu wanakatwa kiasi kwamba wanakosa hata nauli ya kurudi nyumbani mshahara ukichelewa.

Mkopo unaweza kuwa funguo yako ya uhuru na ukuaji kiuchumi ama kifungo na chanzo cha matatizo kwako.






Sent from my TECNO WX3 using JamiiForums mobile app
 
Upvote 1
Back
Top Bottom