Shantel umeandika jambo la maana sana. Kujithaminisha mwenyewe ni jambo la busara sana. Bahati mbaya, ni wachache mno wenye uwezo wa kulitambua hilo. Tatizo linaanzia kwenye maamuzi ya mtu na mtu. Ukishajikubalisha Mwanadamu mwingine akuamulie maamuzi yako, naamini taratibu utaanza kupoteza uwezo na thamani ya maamuzi yako. Hilo litapelekea kuanza kupoteza uwezo was kujiamini (Confidence & Self esteem)
Mfano;
Ni rahisi sana kwenye mapenzi mtu akakujengea hisia hakuna mwingine kuliko wewe. Hakuna ubaya katika kulitambua hilo, ubaya ni pale nawe utaposhindwa kujithaminisha kiukweli uwe mbora kuliko mwingine.
Kimtazamo wangu, kila mmoja wetu amejaaliwa mazuri fulani ambayo yanamtofautisha na mwingine. Mtu atapokupendea kwa mazuri yako, wapaswa nawe kuyajenga na yale ulokuwa na upungufu nayo ili uweze kujikamilisha japo kwa asilimia kubwa zaidi.
Lakini vile vile, ...kuna watu ambao ni mahodari kuwakatisha tamaa wenzao. Watakuja na hadithi za, 'hujapendeza!' 'hujaelimika!' 'huna hoja!' 'hujui hili na lile' nk nk nk.... Ikiwa nawe ni mdhaifu, uka ya accomodate mawazo ya nje yakutawale maamuzi yako, jijue unajichimbia kaburi la kutaka kum- please mtu, ilhali unajipotezea Values zako.
Negative comments ni Challenges za kukupima uwezo wako, "thamani yako!"
Spot on ndugu yangu!...kujikweza kunatuharibia sana ndugu yangu. Tatizo la kujikweza hapafu watu wakaja kubaini mapungufu yako, kunawapelekea wengi kupatwa na msongo mkubwa wa mawazo, na hata wengine kujionea bora wakatishe maisha kuliko aibu watayoipata.