Da vinci jr
JF-Expert Member
- Mar 12, 2012
- 202
- 34
Soma faida za kulala mchana
Je, Unajisikia mchovu, dhaifu na unashindwa kusoma au kufanya kazi mchana? Unatumia soda, kahawa au vinywaji vya kuongeza nguvu kukusaidia kumaliza siku yako kazina au shuleni,
unapiga miyayo masaa yote na kushindana na hali hii? Cha kushangaza ni kuwa suluhu ya hili ni kitu kilekile ambacho tunashindana nacho siku nzima. Usingizi.
Ukweli ni kwamba usingizi ndio njia sahihi kuliko zote ya kurudisha ubongo wako katika hali nzuri ya kufanya kazi mchana.
Kuna Hatua nne kuu za usingizi/kulala. Hatua mbili za kwanza zinakuwa na usingizi mwepesi, hatua ya tatu inakupeleka kwenye usingizi mzito na ya nne unakuwa na kasi kubwa ya macho yaani REM.
Faida za kulala zinategemea sana hatua unazo pitia katika usingizi wako.
Usingizi wa nusu saa unakuruhusu kupitia hatua mbili tu za kwanza za usingizi. Katika hatua ya kwnza unakua na kasi ndogo sana ya macho,
na uki amshwa kwenye hatua hii hujiskia kama haujalala kabisa. Lakini unapo endelea katika hatua ya pili, ubongo wako unapuuzia mambo ambayo unadhani sio ya muhimu na vile ambavyo unadhani havina madhara kwako, Ili uweze kupumzika na kupata usingizi mzuri.
Katika hatua hii pia ubongo una anza kuimarisha kumbukumbu, mambo uliyo fanya au kusoma yanapitiwa upya na ubongo na kupangiliwa.
Kuamka baada ya hatua hii ya pili kumeonekana kurejesha uwezo wa kufanya kazi na kuongeza ufanisi katika kazi au masomo.
Kuongezeka kwa uwezo wa utambuzi, uwezo wa uzalishaji, kumbukumbu, ubunifu na pia la muhimu kuliko yote unapunguza uchovu kwa kiasi kikubwa.
Wanao lala hadi hatua ya 3Kulala zaidi ya dakika 30 hukufikisha hatua ya tatu (3). Ukiamshwa katika hatua hii utakuwa mchovu na utatamani kuendelea kulala. Watu wengi husema kuwa kulala mchana hakuna msaada kwao, lakini ukweli ni kuwa wamelala muda mrefu zaidi.
Wenzetu wa Japani wameligundua hili, ndio maana wamefungua vituo kadhaa jijini humo vya kupumzika mchana kwa wanafunzi au wafanya kazi ili kuongeza ufanisi katika shuhuli zao.
Kwahiyo inawezekana ni vizuri kulala kazini kidogo. Muambie bosi/mwalimu wako sayansi imekushauri ulale.
Kituo cha kulala mchana Japani.Una swali? uliza katika ukurasa wetu wa facebook/masayansi au kwenye kiboxi cha reply hapo chini. Pia usisahau kubofya pua kwenye ukurasa wetu na kushirikisha rafiki zako.
Aksante sana.
Chanzo: Tinomasayansi Blog


