Unajua athari ya tabasamu lako kwa mke wako?

Kama Mungu amekili mwenyewe hawa viumbe jau tuish nao kwa red alarm......God sio mjinga
 
Nimejaribu kuassume hapa yule dada wa kimeru ninavyompa tabasam kila mara naona ni swala ambalo haliwezekani
Inawezekana tabasamu lako Luna makosa ya "kiufundi".

Fikiria, wanyama kama mbwa, samaki, n.k., wanafundishwa na "muelimika', sembuse binadamu?

Unaweza "kumfinyanga" mke wako kwa kutumia upendo.
 
Huyo mke wako ulimwoa akiwa bikira? Tuanzie hapo kwanza. Ukute unatumia energy kubwa kufurahisha zimwi humo ndani afu anakuchora tu.
 
Inawezekana tabasamu lako Luna makosa ya "kiufundi".

Fikiria, wanyama kama mbwa, samaki, n.k., wanafundishwa na "muelimika', sembuse binadamu?

Unaweza "kumfinyanga" mke wako kwa kutumia upendo.
Tatizo lako huna akili. Hatuna namna ya kukusaidia. Tayari una psychopathy disorder.
 
Kama Mungu amekili mwenyewe hawa viumbe jau tuish nao kwa red alarm......God sio mjinga
Ni kwa nini Mungu kasema hivyo? Ni kwa sababu wanawake wana akili. Usipimteka kwa upendo, anaweza akakuuza bila wewe kujua.

Na kwa kuwa umenukuu na Andiko, ni vyema kuendelea na Maandiko.

Waefeso inasemaje? MPENDE MKE WAKO KAMA MWILI WAKO.

Ukifanikiwa kumpenda kama unavyoupenda mwili wako, hautakosa kula matunda mema ya upendo wako.
 
Dunia hapa ilipo kwa sababu ya tamaa za mwanamke...
 
waambie wasisahau kumpa na hela.

Sent from my Redmi Note 8 using JamiiForums mobile app
Au kama hela hamna wajitahidi wampe Dollar

Au kama kuna kidhahabu chochote hata cha kilo 2 we mpe tu kitamsogeza kwa siku kadhaa.

Hata siku ua birthday yake ukimpa zawadi ya Harrier sio mbaya

Ndio uzuri wa wanawake Mungu kawajalia yani wanaridhika kwa vitu vidogovidogo
 
Uchizi huwa unaanza na kuchekacheka hovyo, tabasamu kila mara ni sawa na dalili za uchizi.

Mapenzi yana kanuni, ila maranyingine hizo kanuni huwa zinafeli vibaya.

Utajichekesha na bado atakuona nyau tu...akiwa na jambo lake atalifanya tu ( elewa neno JAMBO).
 
Kimsingi, mwanaume ni mtoaji na mwanamke ni mpokeaji. Lakini, utoaji na upokeaji si kwa mtazamo uliouwasilisha kwenye comment yako.

Hahitaji "kuhongwa" vitu. Anahitaji "kupendwa".

Mwanamke ana gepu kubwa sana linalohitaji kujazwa kwa upendo. Unaweza ukatoa vitu bila upendo na isisaidie kitu, lakini huwezi ukapenda bila "kutoa"
Kutoa kwa upendo, iwe ni kitu au tendo ndiko kutakakoleta matokea chanya.
 
Mpaka dakika hakuna anayejua watakacho wanawake
 
Ukitabasamu tu utaulizwa maswali dabodabo
1. Umeshapata mchepuko mwingine eeh?
2. Umepata hela hutaki kuniambia eeh ?
 
Kuchekacheka hovyo ni tatizo, kadhalika na kutabasamu bila kujua sababu ya kufanya hivyo.

Nilichoelekeza kwenye uzi ni kutabasamu kwa malengo.

Si tabasamu linalochochewa na hisia, bali la kiutuzima. Ni tabasamu linalotawaliwa na ufahamu.

Unatabasamu, si kwa sababu unajisikia hivyo, bali kwa sababu umechagua kufanya hivyo kwa sababu maalum.

Na kwa sababu ni tabasamu ambalo linatawaliwa na ufahamu wako kwa asilimia mia moja, utajua mazingira ya kutasamu na ya kufanya vinginevyo. Siyo unakuwa kama "robot" lililosetiwa.

Ni jambo linalotawaliwa na uamuzi wako kwa asilimia mia moja.
 
Mm hakuna mwanamke na mdate asinipende na tabia yangu ni niko serious mda mwingi na nawaza sana hela .sijawah kuwa nampigia simu mwanamke sijui uko wap sijui nakumiss big NO .
Ni vizuri sana mkuu. Lakini usije ukaleta mada hapa kuomba ushauri ooh nishaurini nimechapiwa!
 
Mpaka dakika hakuna anayejua watakacho wanawake
Wanachokitaka ni jambo moja. Na wanachokihitaji ni jambo jingine.

Wanachokihitaji na wanachokitaka ni vitu viwili tofauti. Kati ya hitaji kuu la mwanamke ni upendo. Hilo ni sehemu ya asili yake. Anao uhitaji mkubwa mno wa upendo kuliko kitu kingine chochote. Na sababu mojawapo ni kwa sababu na yeye anao uwezo mkubwa wa kuuto.

Na ujue, chochote utakacompa mwanamke, atakurudishia kikiwa kimekuzwa zaidi. Ukimpa huzuni, atakurudishia ikiwa imechakatwa na kukufanya uhuzunike kumzidi.

Ukimpenda atakunyenyekea.
 
Watu hawajamwelewa mtoa mada hata kidogo
Unasema mpe hela mpe hela, niulize je inamaana muda wote huo wa mwezi wa zoezi la tabasamu utakuwa hutoi matumizi? Jibu ni hapana

Je unapotabasamu unafanya hivyo bila sababu ya msingi? Jibu ni hapana

Wapo mnaosema kuishi na m2anamke kwa akili , lakini ukiangalia utajua kuwa hilo zoezi ni la kutumia akili na si kukurupuka tu hapo akili inatumika ila hilo hamlioni kwa nini kwa sababu hizo akli mnazonadi zitumike nyie wenyewe hamna na kama mnazo basi hamzitumii!!

Jaribu kumsoma mtoa mada kwa akili ya kuhoji na sio kwa sababu wewe teyari una jibu lako kichwani au makariri fulani uliyokariri ukasahau kuwa hata hao wanawake ni (dynamic na sio static)

Mtu unabeza nguvu ya upendo kumbe hata upendo wenyewe huujui, unapiga kelele hela hela hela ajabu hela nayo huifahamu!!
 
Umeoa mkuu? Tuanzie hapo ili tuongelee from experience. Tumeamriwa kuishi nao kwa akili wewe wekeza hisia kila MTU na mke wake na maisha yake
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…