Daktari wa Instagram
Member
- Jul 9, 2015
- 23
- 2
Unajua jinsi ya kuhesabu mateke ya mtoto tumboni?
Kila mwanamke mjamzito anapaswa kujua jinsi ya kuhesabu idadi ya mateke ya mtoto wake.
Mtoto mwenye afya nzuri HUCHEZA; hujinyoosha, hupiga teke, hujigeuza kila siku,haswa baada ya mama kula au kufanya shughuli ndogo ndogo.
Kuna wakati mtoto hutulia - anapokua amelala.
Mtoto huanza kucheza mimba inapofikia umri wa wiki ya ishrini na nne (24)
Jinsi ya kuhesabu:
1) Hesabu mara moja kwa siku, inashauriwa uhesabu muda ule ule kila siku, pia inashauriwa iwe ndani ya masaa mawili baada ya kula. Wakati wa jioni baada ya chakula ni muda mzuri maana mtoto hucheza zaidi.
2) Chukua karatasi na kalamu kwa ajili ya kueka alama mtoto anapocheza
3) Tumia saa ya mkononi, au ya ukutani kujua muda.
4) Lala ubavu wa kushoto
5) Andika muda wa kuanza
6) Hesabu na weka alama kila anapocheza
7)Hesabu hadi unapofikia mara kumi
8) Mtoto anatakiwa acheze angalau mara 10 ndani ya masaa mawili (2 hrs), lakini anaweza kucheza zaidi ya yapo-zaidi ya mara 10 ndani ya muda mfupi.
9) Andika muda aliofikisha mateke 10.
Mtafute Daktari au Mkunga kama:
1) Mtoto hajacheza siku nzima
2) Kwa siku zinazofululiza, inamchukua muda mrefu zaidi mtoto kucheza mara nne.
3) Inamchukua zaidi ya saa moja mtoto kucheza mara nne.
Naomba unifollow kwenye account yangu ya Instagram...@ daktari_sundae