Kuna kampuni inaitwa Highway Carriers ya Azim Dewji na nduguze, ilikuwa inahusika na mambo ya Freight and Carco clearance na Transporatation.
Babangu kafanya kazi hapo kwa karibu 10 siku alipoamua kuacha kazi niliamua kwenda NSF kuulizia mafao yake nikakuta Highway hawalipi NSSF na wapo Dar. Mzee akaamua kususa hata mafao yake ya zamani ya NSSF (PPF) maana tangu 1967 hadi 1986 akiba zilikuwa 400,000/- (Laki nne) sasa hao NSSF wenyewe wanatuibia kwa kutoangalia thamani ya pesa ambayo babangu alianza kuweka miaka ya 1960 mshahara ukiwa shilingi 10 na hadi mwaka 1986 ana 400,000/- (pamoja na faida), kama si mzaha ni nini?
NSSF sidhani kama wataweza kutusaidia dhidi ya wizi wa Waajiri wetu. Mfano mdogo tu, mimi nina akiba ya NSSF shs 8,000,000/- hadi June 2006 na nikakuta faida walonipa ni shs 6,000/- tu. Sasa sio wizi huo? Mapesa yetu wanapeleka wapi au ndo hizo Serikali yajichotea tu kwenye chaguzi?
Ok, pamoja na hayo nimekupa Jina la Mwajiri ambaye hapeleki michango ya Wananchama tangu 1987 hadi 1996. nasubiri bingo yangu.