Cytochrome p450
JF-Expert Member
- Mar 19, 2019
- 5,638
- 15,044
Kama uliwahi kujiuliza hili swali, basi jibu lipo hapa..
Mambo yoote yanaanzia kwa huyu mwanamama anaekwenda kwa jina la Florence Nightingale. Huyu anatambulika kama muuguzi wa kwanza kabisa duniani na ndie mwasisi wa kozi ya uuguzi.
Kwa wale wenzetu wa mambo ya uuguzi, jina hili sio geni kwao.
Sasa story inaanzia kwenye miaka ya 1853, wakati wa vita ya krimea (The Crimean War) kati ya Waingereza na Warusi.
Vita hiyo waingereza waliumia vibaya na kipindi hicho hawakuwa na madaktari wa kijeshi.
Taarifa ziliandikwa sana kwenye magazeti ya kipindi hicho na zikawafikiwa watu wengi akiwemo bibie Florence.
Basi huyu mama akaamua kuandaa timu yake ya wanawake 38, kisha kuwapa misingi ya namna ya kuwahudumia wagonjwa. Wakatia timu kambini na kufanikiwa kuokoa maisha ya wanajeshi wengi kipindi hicho.
Baadae serikali ya Uingereza ikaamua kujenga vituo vya kufundishia wauguzi na wote waliokuwa wakijiunga ni wanawake.
Tangu kipindi hicho, hii kazi ikawa ni kwa ajili ya akina mama pekee.
Siku hizi mambo yamebadilika wakuu, mpaka wakaka wanafanya!😁