Unajua mapishi ya samaki pweza????

Unajua mapishi ya samaki pweza????

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2009
Posts
42,872
Reaction score
34,363

SAMAKI HUYU NI MTAMU SANA IKIWA UTAPATIA JINSI YA KUMPIKA NA MAPISHI HAYA HAYA UNAWEZA TUMIA PRAWNS WA AINA ZOTE, LOBSTA, CHAZA NA UDUVI IWE NI KUTENGENEZA MCHUZI SAFI AU KUTENGENEZA SUPU HATUA ZA MAPISHI NA MAHITAJI NI HIZI HIZI

MCHUZI MZITO WA PWEZA

MAHITAJI

70 gram kitunguu swaumu
150 gram kitunguu maji kata kata
150 gram karoti kata vipande vidogo
1 pilipili ya kijani fresh a pili pili mbuzi
1 kijiko kidogo cha chai unga wa korienda au girigilani
200 gram viazi ulaya
10 gram chumvi
150 gram pilipili hoho
160 gram mafuta ya kupikia
70 gram juisi ya limao
500 gram nyanya ya kopo
350 gram Maji
1 kilo ya pweza kata kata vipande vidogo vidogo

JINSI YA KUANDAA

Weka mafuta katika sufuria kisha acha ya pate moto baada ya hapo weka kitunguu maji kaanga kwa dakika 1 kisha weka kitunguu swaumu kaanga tena kwa dakika 1 kisha weka pweza na viazi ulaya kaanga kwa dakika 10 - 15 kwa moto wa wastani.
kisha weka unga wa korienda, caroti, pili pili hoho, chumvi, pili pili mbuzi, juisi ya limao kaanga kwa muda kisha weka nyanya ya kopo koroga vizuri kisha weka maji acha ichemke kwa dakika 5 mchuzi upungue itakua imeiva.

JINSI YA KUANDAA SUPU YA SAMAKI PWEZA ( OCTOPUS)

1 Samaki pweza mkate na msafishe vizuri
50 gram kitunguu swaumu
100 gram kitunguu maji chop chop
100 gram kariti kata vipande vidogo
1 pilipili ya kijani fresh
1 kijiko kidogo cha chai unga wa korienda au girigilani
5 gram chumvi
5 gram pilipili manga
100 gram mafuta ya kupikia
50 gram juisi ya Limao
150 gram nyanya ya kopo
1.5 lita ya Maji
1 kilo ya pweza

JINSI A KUANDAA

Weka mafuta katika sufuria kisha kaanga kitunguu maji na kitunguu swaumu baada ya hapo weka pweza kaanga kwa dakika 10 kisha weka viungo vyote vilivyobakia kaanga kidogo kisha weka maji chemsha katika moto wa wastani kwa dakika 15 itakua imeiva mpatie mlaji ikiwa ya moto

Huu ni muonekano wa samaki pweza akiwa amekatwa na kusafishwa vizuri

SUPU YA PWEZA YENYE LADHA YA NYANYA NA LIMAO

KWA WALE WASIOTUMIA NYANYA KWA MATATIZO YA GESI NA KIUNGULIA USIWEKE NYANYA YA KOPO NA SUPU YAKO ITAKUA NA MUONEKANO HUU NA LADHA SAFI KABISA.cc farkhina cc TUKUTUKU cc BAK
 
Mhhhhh! Dr MziziMkavu mpaka kwenye mapishi pia!!!! Dah weye MKAREEE mie nilifikiria kwenye zile kwato za fisi tu na manyoya ya mkia wa tembo 🙂🙂 ndio utaalamu wako ulikolalia kumbe mpaka mekoni upo!!! dah!!! Hongera zako. Huwezi kulala na njaa kwa kula majunk food.
 
Last edited by a moderator:

Kuna siku alinirusha roho huyo alipika mchuzi wa samaki hadi nkauota lol..

Vipi lile pishi la pilipili bado unaendelea?

Sent from my BlackBerry 9320 using JamiiForums
 
Last edited by a moderator:
lol!!!!! yaani unaota mapishi mpaka usingizini dah!!!!

[/SIZE][/FONT]
Kuna siku alinirusha roho huyo alipika mchuzi wa samaki hadi nkauota lol..

Vipi lile pishi la pilipili bado unaendelea?

Sent from my BlackBerry 9320 using JamiiForums

lol!!!!! yaani unaota mapishi mpaka usingizini dah!!!! Wanaume wengi wa miaka hii hawaoni nomaa kuingia jikoni kufanya vitu vyao ukilinganisha na ile miaka iliyopita. Na kama mnaishi nyumba yenu na si zile [/FONT]za kupanga za vyumba sita basi zoezi la mwanaume kuingia jkoni linakuwa rahisi zaidi.

Umeona eeh BAK...

U r real gentleman...

Sent from my BlackBerry 9320 using JamiiForums
 
Last edited by a moderator:
Majunk food yalinishinda ikabidi nijue kupika angalau vyakula vichache na hivyo vyakula vichache nimekuwa ni mtaalamu.

Umeona eeh BAK...

U r real gentleman...

Sent from my BlackBerry 9320 using JamiiForums
 
Unakula ugali weye!!! hahahahah lol!!! na nyama ya kuchoma kwa kachumbari? Kama huna matatizo basi karibu sana..😛lane:

Hebu nialike siku moja nije nionje mapishi yako....

Nsije tu kujing'ata vidole kwa utamu lol...
 
Mhhhhh! Dr MziziMkavu mpaka kwenye mapishi pia!!!! Dah weye MKAREEE mie nilifikiria kwenye zile kwato za fisi tu na manyoya ya mkia wa tembo 🙂🙂 ndio utaalamu wako ulikolalia kumbe mpaka mekoni upo!!! dah!!! Hongera zako. Huwezi kulala na njaa kwa kula majunk food.
Hakika Mungu amemjalia vipaji vingi!
 
Kuna siku alinirusha roho huyo alipika mchuzi wa samaki hadi nkauota lol..

Vipi lile pishi la pilipili bado unaendelea?

Sent from my BlackBerry 9320 using JamiiForums
Ukiolewa na huyu jamaa utafaidi sana maisha!
 
Unakula ugali weye!!! hahahahah lol!!! na nyama ya kuchoma kwa kachumbari? Kama huna matatizo basi karibu sana..😛lane:

Ugali Ntakula ivo ivo kufuata hiyo nyama lol...na kachumbari napenda sana
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Back
Top Bottom