JamiiTalks
JF Advocacy Team
- Aug 7, 2018
- 685
- 1,124
JE, UNAJUA DHUMUNI LA KARANTINI?
Karantini ni utaratibu unaotumika kipindi cha magonjwa ya mlipuko ili kuzuia au kupunguza kiwango cha kusambaa kwa magonjwa
Katika kipindi hiki ambapo dunia inakabiliwa na #COVID19 wasafiri kutoka nchi moja hadi nyingine wamekuwa wakiwekwa karantini kwa muda wa siku 14
Nini faida au dhumuni la karantini?
1. Kufuatilia afya ya mshukiwa wa ugonjwa husika na kumpa huduma stahiki. Ndani ya siku 14, endapo mtu huyo ameambukizwa, dalili zitajionesha na ataweza kupatiwa msaada wa haraka
2. Kuzuia maambukizi kwenda kwa jamii. Endapo mtu ameambukizwa, anaweza asioneshe dalili na akienda kuchangamana na watu wengine anaweza kuwaweka kwenye hatari kwa kuwaambukiza ugonjwa
Upvote
0