Unajuta kumfahamu au? Tumbua jipu hapa

dalalitz

JF-Expert Member
Joined
Sep 6, 2013
Posts
3,423
Reaction score
1,987
Habari Waungwana?

Bila shaka tutakubaliana kuwa kukutana katika
Mitandao ya kijamii kwa wengine kumepelekea
Ukaribu wenye tija, faraja na wa-kuenziwa

Hata hivyo, Binadamu tuna mengi,
Ni kwa mukhtadha huohuo basi,
Yawezekana mkafahamiana kupitia
Mitandao hiihii lakini mkatengeneza
Uadui,Kero,Usumbufu,Chuki au
Majuto yasiyoweza kusahaulika
Kirahisi maishani.

Tuzungumzie hapa MMU ya JF.
Bila kujali ni nani,kuogopa au
Kulindana,
'LIVE' Kabisa ieleze jamii ya jukwaa letu pendwa;
Memba gani kakukuna, anaendelea kukukuna pengine na hujawahi
Au pengine HUJUTII kumfahamu?

Lakini pia, Kuna wale Wazee wa KERO,
Waweke hadharani kwa majina na kero zao.

Ni mwendo wa PONGEZI NA KUTUMBUA MAJIPU UCHUNGU.

Nawasilisha.
 
Kaka jambaz ni mmoja wa watu ppwa kwangu mshana jr na madam na vidda viwili
 
Kuna watu wananikera kwa kupenda pesa sema wanamidomo haoooo. Ngoja nimezee tu ila sio poa wajierekebishe
 
Katika maisha hakunaga nafasi ya kujuta. Wale waliokufurahisha ama kukusaidia wamekufunza umuhimu wa kuwa mtu mwema, waliokuumiza wamekufunza umuhimu wa kuwa mwangalifu na pia kutoumiza wengine.
 
What happens in Vegas stays in Vegas.......
 
Na ili aelwe vizuri practical muhimu....

Kwa upande wangu miye nafarijika sana kwa Huyu bibie Brenda 18 amenifanya nianze kufuta vumbi kuifuata furaha niliyokuwa nimeipoteza
 
Kwa upande wangu miye nafarijika sana kwa Huyu bibie Brenda 18 amenifanya nianze kufuta vumbi kuifuata furaha niliyokuwa nimeipoteza

Hongera mkuuu, huyo anaitwa dr BRENDA 18
 
Last edited by a moderator:
Hongera mkuuu, huyo anaitwa dr BRENDA 18

Yeah! Lakini huwa hatupendi kulitumia hilo la Dk.. Nafarijika kila nisomapo alichokiandika... Usishangaa nikakwambia nipo kanda ya Ziwa.... Hakika Mungu ni Wakushukuliwa
 
Last edited by a moderator:
Yeah! Lakini huwa hatupendi kulitumia hilo la Dk.. Nafarijika kila nisomapo alichokiandika... Usishangaa nikakwambia nipo kanda ya Ziwa.... Hakika Mungu ni Wakushukuliwa

Karibu mkuuu, mi pia nipo huko....ha haaaaa.....
Umeahirisha ile mishe ya kili town
 
 
 
Mshana jr,laki si pesa,miss chaga wamefanya nijiunge jf
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…