Teknolojia ni Yetu sote
JF-Expert Member
- Apr 28, 2020
- 620
- 1,240
Kampuni ya Austin imetengeneza choo cha kisasa chenye kamera📸 kwa ajili ya afya yako 😲. Unaweza sema wamechanganyikiwa awa jamaa au lah lakini ndo uwalisia sasa.
Teknolojia hiyo mpya inaitwa throne, ambayo kwenye choo unaweka kamera ambayo inapiga picha ya kinyesi chako. kupitia Teknolojia ya AI au Akili bandia inafanya Kazi ya kuchambua kinyesi chako na kukupa taarifa ya afya yako kuhusu tumbo lako nk.
Kampuni hiyo imeweka kamera kwenye sinki la choo ambalo yenyewe inafanya Kazi ya kupiga picha zile harakati zako zote za haja kubwa, kwa kutumia Teknolojia ya AI au Akili bandia na kukusaidia kujua afya yako kuanzia afya ya mwili na unyevu nyevu kwenye kinyesi
KUMBUKA
🛡️ Kamera ndogo inawekwa kwenye choo na kuchukua taarifa ya kinyesi chako
🛡️ Picha huweza kuchambua kinyesi chako kupitia algorithm ya AI ambayo inatambua mfumo mzima wa afya yako ya utumbo, kiwango cha maji kulingana na kinyesi ulichokitoa.
🛡️ Taarifa zote zinazotolewa kukuhusu wewe zitakua za Siri na salama kwani kampuni azitaweza Siri za mteja wao.
🛡️ Watumiaji wataweza kuona taarifa za vinyesi vyao na taarifa mbalimbali kupitia app yao.