[Mwanameka -Dar International(Marijani)]
[Wote]
Kweli penzi eee, penzi lavunja udugu
Watu wakakorofishana, wakakosa kusikilizana
Penzi lavunja unyumba eee, nimeyaona kwa Musa
Mwanameka umeleta maneno, umeuvunja unyumba kwa Musa
Mwanameka eeee, Mwanameka jirani yangu
Mimi naona vibaya.......
Umemponza mamaye , umemponza mwenzio
Mwanameka umeleta maneno, umeuvunja unyumba kwa Musa
Uliposikia eee, kwamba Musa ameoa
Kaoa mke wa ndoa.......
Musa sasa katulia eee, uhuni kaweka kando
Ukatumia kila uwezo, kuyabadili mawazo ya Musa
Watambua eee,ukifusa(?) urembo
Ukazidisha na mapambo, vipini wanja kwa poda eee
Na mwendo wako maringo...
Musa macho yake yameona, na moyo ukaanza sononeka
Ukabadili na njia eee. lazima upite kwa Musa
Ukenda sokoni kwa Musa....
Musa amevumilia eee, mwisho kapotea njia
Kakusimamisha bila kutambua, akazungumza neno la mapenzi
Ulipopata kauli yake, ukakubali bila kusita
Uliyotaka yamekuwa......
Kazi ikawa ni moja, ni mapenzi motomoto
Umempa pendo lenye huba, maneno matamu kama asali
Ukichanganya na urembo wako, Musa kanasa kwenye ulimbo
Akili zake zimemruka...
Kwako wala habanduki, kwa mkewe hakumbuki
Amekwisha ionja asali, anataka kuchonga mzinga
Penzi nalo eee, penzi nalo halina siri
Na siri si ya watu wawili...
Mkewe Musa katambua, naye kadai talaka
Hakuliki wala hakulaliki, mpaka Musa katoa talaka
Baada ya kisa eeee, Mwanameka umefanya mkasa
Kweli wanisikitisha....
Mara Musa humtaki, hata kumuona hupendi
Jama Musa ameumbuka, kakosa mwana na maji ya moto
Kweli penzi eee, penzi lavunja udugu
Watu wakakorofishana, wakakosa kusikilizana
Penzi lavunja unyumba eee, nimeyaona kwa Musa
Mimi sasa nimeshaamini, Ibilisi ya mtu ni mtu
(Chorus)
[Wote]
Kweli Mwanameka umefanya madhambi makubwa
Mambo ulomfanyia Musa yanasikitisha
Eee Mwanameka mkasa uliofanya ni wa mwaka
Ooo bwana Musa hatokushau mpaka kufa
Tena amekwisha apa mambo ya upuuzi hataki tena
Keshaumwa na nyoka akiona unyasi anashituka
Eee Mwanameka hebu punguza matata
[Marijani]
Mwanameka umetuachia hadithi mitaani
Kila mmoja anashangazwa na vitendo vyako
Kila mtu anasimulia mambo yako
Ati watu mama wanasema.......
[Wote]
Mgombanishi....
[Marijani]
Kweli watu mama wanasema....
[Wote]
Muhuni
[Marijani]
Ati watu mama wanasema.......
[Wote]
Mdanganyifu
[Marijani]
Kweli kweli kweli Mwanameka....
[Wote]
Umezidi
[Marijani]
Oooooooo Mwanameka
[Wote]
Umezidi
[Marijani]
Mwanameka umetuachia hadithi mitaani mama aaa
[Wote]
Kweli mwnameka umefanya madhambi makubwa.........
YouTube - Marijani Raajab - Mwanameka