MT255
JF-Expert Member
- May 3, 2012
- 3,606
- 4,914
Gololi ni mchezo wa watoto wa zamani ambao enzi hizo ulichezwa sana... Gololi kubwa sana iliitwa “Dungu” na Gololi mpya iliitwa “Kinyuli” Gololi iliyokuwa imemeguka iliitwa “Betri”.
Shimo la kuchezea Gololi liliitwa “kibweshi ” pale Gololi ilipoingia ndani ya kibweshi na kutoka unasema “Umekula” Mchezo ulikuwa ni kulenga mara mbili na ukilengwa mara zote tunasema “umeliwa” (Unatakiwa kumpatia mwenzako Gololi nyingine) kama ukilengwa na kelele haikutoka ulikuwa utata balaa... wabishi na watemi walikuwa ndiyo kichaka chao.
Gololi za Chuma hazikuruhusiwa kabisa na kulikuwa na gololi aina fulani hivi nyeupe zilikuwa adimu sana kupatikana...zilikuwa zinaita TEMBO....dah wakati umeenda sana watoto wa leo hawajui hii kitu[emoji23][emoji23]
Enzi za gololi ulikuwa wapi mtu wangu?