Unakumbuka mchezo wa gololi?

MT255

JF-Expert Member
Joined
May 3, 2012
Posts
3,606
Reaction score
4,914
Gololi ni mchezo wa watoto wa zamani ambao enzi hizo ulichezwa sana... Gololi kubwa sana iliitwa “Dungu” na Gololi mpya iliitwa “Kinyuli” Gololi iliyokuwa imemeguka iliitwa “Betri”.

Shimo la kuchezea Gololi liliitwa “kibweshi ” pale Gololi ilipoingia ndani ya kibweshi na kutoka unasema “Umekula” Mchezo ulikuwa ni kulenga mara mbili na ukilengwa mara zote tunasema “umeliwa” (Unatakiwa kumpatia mwenzako Gololi nyingine) kama ukilengwa na kelele haikutoka ulikuwa utata balaa... wabishi na watemi walikuwa ndiyo kichaka chao.

Gololi za Chuma hazikuruhusiwa kabisa na kulikuwa na gololi aina fulani hivi nyeupe zilikuwa adimu sana kupatikana...zilikuwa zinaita TEMBO....dah wakati umeenda sana watoto wa leo hawajui hii kitu[emoji23][emoji23]

Enzi za gololi ulikuwa wapi mtu wangu?
 
Gololi zilinifanya kushika mkia darasani kipindi hicho hakuna nilichowaza zaidi ya gololi mpka leo zimenipa Uzero IQ
 
Tukiita nguti hiyo ilikuwa Songea 1983-1985 hahaa hii kitu ilisababisha niwe nachapwa Takriban kila siku Sababu nikitoka shule badala ya kurudi home tunaanza cheza nguti mara saa 12 jioni na nyumbani kuna bustani inanisubiri kumwagilia
 
mecheza sana makwemeee.....ukilenga ya kutoshaaa ...unakimbilia home unaenda yakaanga unajipongezaaa
 
Kuna gololi iliobanjuka hapo
 
Hapa hakuna cha Ps 4 wala cartoon,ni kuchimba vishimo na kulenga,mpaka ukiambiwa chakula tayari unaona kama vile unaitwa kupewa sumu..
 
Daah mi nakumbuka gololi mpya ilikuwa tunaita "kimma au kinywesti" halafu zile zilizochakaa tunaita "mabanju" yani ilikuwa mtaani watoto wengi sana wanatoka mitaa ya mbali wanakuja mtaani kwetu yani hapo zinasikika kelele tu mtu hakumbuki hata kwao labda "akifuswa "ndo huyo mdogo mdogo kwao aiseee ilikuwa noma sana kipindi hicho
 
Tulikuwa tunaiita hiyo kitu JAGA...

Acha kabisa aiseeee, maisha yalikuwa matamu sana
 
Kinyulaa,gweraa,kiksi,dungu dunguu,masala,kidu,no kiksi,no kila,no riba,no mdondo
Hizo ni baadhi ya misemo tu ninayokumbuka chuga enzi hizoo
 
Hapo ni Mwanza miaka ya mapema 90 hata la kwanza sijaanza ilikuwa ukimwambia mtu Itachaji ni ugomvi, maana hata ukipiga mchanga ikaguswa umempuna
 
Unanikumbusha mbali mtaani kwetu jamaa wakiniogoma kinoma kwa shebaha za kutunga gololi wakiona na mimi nahitaji wananikataza kwa sababu nitawabanja wote. Hahahahaaa
 
yes kila kitu...no mtingi...no kicks...FULL KINYULAA HAINA GWERAA...VUTA NGASAA.... MPUSA... KIDU....NIKOROGEE MASALA
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…