Kichwa Kichafu
JF-Expert Member
- Apr 13, 2017
- 44,855
- 189,385
Leo kwenye shughuli na mihangaiko ya kila siku nikakutana na vijana wakipiga shangwe, kelele na kila aina ya hamsha hamsha unazozijua za vijana wa sasa.
Ndipo nikamuuliza mwenyeji wa eneo hilo kulikoni? Ndipo aliposema ni watoto wa form four wana sherehe za kumaliza shule.
Hapo ndipo nikakumbuka mimi kipindi hicho. Nakumbuka nilikuwa naamini graduation kama nikunipotezea muda maana nilikuwa wa kusoma kweli( enzi hizo).
Basi ilivyofika siku ya graduation wala nilikuwa sina habari kama kuna shughuli muhimu ipo shuleni. Nikawa nafata ratiba yangu niliyojiwekea(maisha ya boarding) nikaamka asubuhi nikaenda zangu class kupiga kitabu japo nilikuwa na umakini mchana swala la chakula.
Wali kilikuwa ni chakula special sana kama mnavyokumbuka maisha ya boarding yalivyokuwa.
Sasa wakati wa sherehe sakata likafika kwenye ugawaji wa vyeti na zawadi pale ndio kukaleta mtafaruku.
Kiukweli enzi hizo nilibahatisha bahatisha kuchukua vyeti vingi vya masomo mbalimbali ukiongeza na mbwembwe za waalimu wakaongeza na cha nidhamu. (Kama mwanafunzi bora)
Wakati vyeti vinagawiwa kila wakiita mwanafunzi bora kwenye somo husika sipo.
Hili swala lilileta kama mshangao kwanini huyu mwanafunzi hajatokea wengine wakahisi labda naumwa ikabidi waanze kunitafuta.(waalimu wa zamu)
Walikuja kunipata almost shughuli imekaribia kwisha nikalazimishwa kwenda kuungana na wenzangu japo tayari ilikuwa imefika muda wa kula.
Muda wa picha hata sikutaka kwenda sababu kama walikuwa wamenikurupua nikaendelea na mambo yangu.
Nikawasalimia salimia baadhi ya wazazi wa marafiki zangu maana mimi hata home sikutaka wajue kama kuna graduation.
Kiukweli waalimu wengi walinilalamikia sana wa ushauri walitoa ushauri kipindi hicho. Nilijisikia vibaya sana maana mimi nilikuwa naona ni jambo la kawaida tofauti na wao.
Muda ulivyokwenda nikikumbuka najiona nilivyokuwa Mwehu kwa huu upuuzi niliowahi kufanya.
Wewe unakumbuka nini kwenye graduation yeyote ile katika maisha yako?