Unakumbuka tukio gani la Sergio Ramos?

gekaboy

Member
Joined
Nov 27, 2021
Posts
49
Reaction score
106
Kwenye maisha ya soka ukiachilia mbali mabao na vyengaa ila burudani nyingne ni kushudia utukutu na ubabe wa wachezaji

Sergio Ramos master Red card, kati ya tukio ambalo nalikumbuka kutoka kwake ni umafia kama sio ujambazi aliomfanyia mo Salah kwenye michuano ya UEFA champions
Mwamba kakamata mkono alfu akang'oa stendi ya Salah kilichofata nahisi kila mwanasoka anafahamu

Je ni tukio gani ambalo unamkumbukia mwamba Ramos akiwa na Uzi wa Madrid pamoja na timu ya taifa ya Spain?

NB: alishawahi kumwambia velverde akiwa anamfukuzia morata" kill him "[emoji1787][emoji1787]

 
RAMOS ni Mkurya wa Nyamwaga Tarime ndani ndani hukoo. Hayo matukio ya Kibabe ni jadi ya Ukoo wa babake Mzee Ramogi. Vita ni Vita Murra huyo ni kijana wetu tunamjua wenyewe Wacha atwakirishe ayapige mitama mazungu mpaka yatapike kichuriii!
 
Hii picha ni siku niliyofurahi sana
 
Tukio ambalo yeye na Pepe walimfanyia faulo kwa pamoja bwana Messi.


Goli alilowafunga Atletico Madrid dakika ya 92 kwenye fainali ya Uefa ni rekodi nzuri pia.


Kabla ya kufunga goli hilo Atletico walikua wanaongoza kwa goli 1 bila na zilibaki dakika 3 tu watangazwe kua mabingwa wa ulaya.

Baada ya kusawazisha, mechi ilienda mpaka dakika 120 na matokeo yaliisha wa Madrid kumfunga Atletico jumla ya mabao 4 kwa 1 na kutwaa ubingwa.
 
Naikumbuka hiyo mechi alimwagiza Marcelo amkavie nafasi yake akamwambia mpiga Kona amsubirie kama bahati akatia kamba na ndipo upepo ulipo badilika
 
Pamoja na undava wote tusisahau pia ndiye beki mwenye magoli mengi zaidi. Kashatia kambani zaidi ya magoli 100 na bado tutaendelea kuhesabu maana bado anacheza soka.

Ila ile header dhidi ya Atletico Madrid ni ngumu kusahaulika. The Prime Ramos alikua hatari kuliko hatari yenyewe.
 
Kati World cup 2010 ama euro 2008 kama sikosei ndio mchezaji aliyepiga chenga nyingi zaidi kipindi hicho anacheza beki ya kulia.
Game ya kwanza spain word cup 2010 alipasuliwa goli moja na switzerland nakumbuka pique alikua anavuja sana Sergio Ramos akawa anaingia kati kuziba nafsi
 
Nilikua na demu wangu mmoja jina lake lilikua linaanzia na R sasa ili mademu wengine wasijue kinachoendelea basi yule demu nika msevu Ramos, Huyu mwamba alikua katili kwelikweli !!!
 
Ukiachilia mbali kumpiga Messi kiwiko, Madrid wanakufa 3-2 Messi anacheza game na pamba mdomoni.

Juzi Kati baada ya kurudi sevilla, kuna game alicheza rafu refaree kampa yellow card jamaa ana complain kwamba refaree akacheki VAR. Baada ya refaree kucheki VAR ikaonyesha jamaa kacheza bad foul kaishia kula red card
 
Nilikua na demu wangu mmoja jina lake lilikua linaanzia na R sasa ili mademu wengine wasijue kinachoendelea basi yule demu nika msevu Ramos, Huyu mwamba alikua katili kwelikweli !!!
Hamzidi Pepe the Vampire
 
Mimi nakumbuka ile ya Pepe alivyomkita mara mbili Messi na guu lake,jamaa makatili sana hawa.
 
Alivyomfanyia Mo Salah Katika uefa final kati ya Real Madrid na Liverpool.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…