Binadamu ni social animal. Kupiga soga, kushare taarifa na kutoa ni sehemu ya kusocialize.
Sasa unapokuwa hana access ya hivi vitu katika mazingira yake anamoishi ndio mtandaoni kunakuwa kimbilio lake.
Mitandaoni kuna taarifa mbali mbali sasa aina ya akili aliyonayo mtu ndio inaamua aina gani ya taarifa anatafuta.
Mfano watu wanaopenda kufuatilia Maisha ya watu utawakuta wanafuatilia umbea, watu wanapenda maswala ya kifedha utawakuta wanafuatalia taarifa za uwekezaji, watu wanaopenda mambo ya kiimani utaona wanafollow pages za mafunzo ya kiimani, na kadhalika.
So nadhani inategemea na mtu sio wote wanapenda kufuatilia udaku. Kama mimi udaku umenishinda kabisa kufuatilia sababu naona kazi sana kuamka nikiwaza leo nani litakuwa limemkuta lipi ila kuna watu akimka asubuhi kitu cha kwanza anakwenda kwenye page ya mtu fulani anayepost sana matukio ya watu ili akaone kuna jipya lipi asubuhi ya leo.