mwanyaluke
JF-Expert Member
- Jan 22, 2015
- 704
- 2,435
Nimejikuta hivi vyakula ni sehemu ya mlo wangu karibu Kila siku, ukiwa nyumbani utakuta pamepikwa , uingie mtaani hadithi ni Ile Ile, nimevichoka ila sasa sielewei najinasuaje , vyakula hivi ni 1. Wali 2. Ugali 3. Chips 4. Chapati 5. Ndizi na mboga hizi 1. Nyama 2. Samaki( samaki na dagaa) 3. Maharage 4. Mboga a majani marufu kama Chinese, vip unatoboaje na unavikwepaje, je unaweza toboa wiki usikutane na hiyo menu hapo juu,. Nimefanikiwa kukata matumizi ya soda na beverages nyingine nyingi, natumia maji tu ila kuhusu vyakula imekuwa kazi ngumu ,nenda mgahawani kwa mama lishe to hotelini misosi ni hiyo hiyo