Pale mahakamani wanajenga hoja ili kupata mshindi. Hapa tunajenga hoja ili kujenga. Hakukuwa na sababu ya kutaka kubadilisha uelekeo wa uzi kutoka dreads kwenda heleni, wakati una uwezo wa kuanzisha bure uzi wa hereni
Kuna mfano niliuweka hapo mwanzo naomba niutumie na hapa
Mleta mada angeanzisha mada yenye kichwa cha habari kinachosema "unamchukuliaje mtu aliyejikojelea mikojo"
Mpaka hapa hii habari inakua kwenye category ya "ustaarabu"
Halafu kunogesha habari, mtoa mada akaambatanisha na picha ambayo inaonesha mtu kajikojolea lakini pia kajinyea
Moja ya wadau akahoji kwanini mtu huyo amejinyea na hauja sema chochote kuhusu kitendo hicho je ina maana kwako wewe mtu akijinyea sio big issue?
Bila shaka swali litakua ni valid kwasababu lipo katika category moja kuzungumzia "ustaarabu"
Nikija sasa kwenye hoja kuu ya mdau, kwenye ishu ya dread na kwa namna alivyo li-represent ni kama anawaona watu wa namna hiyo ni watu wa ajabu "kimaadili"
Lakini hapo hapo kupitia picha yake, kimaadili imekaaje kwa mwanaume kuvaa heleni?
Kwasababu ishu ya dread unaweza kuitetea kwa hoja nzuri ambazo zikakubalika kimaadili. Tuna watu mitaani wanaimani ya kirastafarian hawa katika dini yao ni lazima kufuga nywele
Unapotaka kumtetea mwanaume anayevaa heleni utatumia hoja gani ambayo itakua supported na kimaadili?