Wild Flower
JF-Expert Member
- Jul 20, 2023
- 378
- 766
Mfahamu Idris Sultan
Amezaliwa Januari 28, 1993 jijini Arusha. Anafahamika kama mwigizaji, Mchekeshaji na mtangazaji wa vipindi vya radio
Safari yake ya mafanikio ilianza baada ya kushinda shindano la "Big Brother" mwaka 2014 na kuzawadiwa zaidi ya milioni Tshs. 514 akiwa na umri wa miaka 22.
Idris Sultan amekuwa Mtanzania wa kwanza kuigiza Netflix katika filamu ya ‘Slay’ mwaka 2021. Na baadaye mwaka 2023 alipata fursa ya kushiriki kwenye filamu nyingine iitwayo ‘Married to Work’ iliyoongozwa na muongozaji mahiri Philippe Bresson
Amewahi kushinda tuzo mbali kama vile:
Mtangazaji wa Vyombo vya Habari Mwenye Mavazi Bora Afrika - 2016
Tuzo za Mitindo na Mavazi za Abryanz - Mwanamume Mwenye Mitindo/Mavazi Bora (Afrika) - 2017