Unamkumbuka Dj Seydou, huyu ndiye Dj aliyepiga ngoma mpya kila akipanda stejini

Unamkumbuka Dj Seydou, huyu ndiye Dj aliyepiga ngoma mpya kila akipanda stejini

MT255

JF-Expert Member
Joined
May 3, 2012
Posts
3,606
Reaction score
4,914
Kunako miaka ya 80 na mwanzoni mwa miaka ya 90, majina ya Ma-DJ yalikuwa makubwa kama ilivyo kwa wanamuziki wa kizazi kipya na cha zamani hivi sasa. Mojawapo ya majina hayo ni DJ Seydou(pichani).

Yeye na DJ mwenzake aliyekuwa anajulikana kama DJ Gerry Kotto walitamba sana na disco lao la RSVP Discotheque pale Mbowe (siku hizi Club Billicanas). Enzi hizo vijana walikuwa waende wanakokwenda usiku unakuwa haujakamilika kama hawatofika Mbowe kupata ladha kutoka kwa DJ Seydou na mwenzake.Jina lake halisi ni Saidi Mkandara.

Tofauti na Ma-DJ wenzake wa enzi hizo, yeye alikuwa sio muongeaji sana. Badala yake yeye alisifika sana kwa uwezo wake wa kupangilia miziki. Akianza vitu vyake alikuwa hakai mtu kitini mwanzo hadi mwisho. Uwezo wake wa kusoma ukumbi na kujua aweke muziki gani ulikuwa unawastaajabisha wengi.

Isitoshe DJ Seydou alikuwa akisifika kwa kupata nyimbo mpya mpya kabla ya DJ yeyote mwingine enzi hizo. Kila jumamosi alikuwa hakosi kuibua kibao ama vibao vipya kutoka kona mbalimbali za dunia.

DJ Seydou alianza shughuli hizi pale Sea View enzi za Sansui miaka ya katikati 70…akipewa muda mfupi sana kwani enzi hizo Afro 70, Safari Trippers walikuwa ndio ngome ya jiji ktk muziki. Maneno yote yalikuwa Princess pale mnazi mmoja.
Nakumbuka mwaka 1980 Dj Seydou akishirikiana na Eddy Sally na Choggy Sly walianzisha disco pale Key's Hotel hapo mjomba hakuna YMCA wala Msasani isipokuwa Mbowe Dj akiwa Gerry Kotto (sio Yafet Kotto), Africana na Seaview.

Nakumbuka walifanya mashindano ya kucheza na mshindi alikuwa Golden hair (Abdallah) na Mosi Ally yule mkimbiaji wetu wa mita 100.
Mwkaa mmoja tu walisambaratika! Choggy na Eddy Sally walikwenda Silversand na Seydou pamoja na Gerry Kotto waliungana kuunda kikundio kipya cha Space 1900 pale YMCA. Hapo ndipo Joe Janson na Kalikali walikuja ibuka hata ilipofika mwaka 1982, Space 1900 walihamia Mbowe. Kule YMCA wakawa wanapiga disco la mchana kwa vijana wadogo.

Space wakafungua tena sehemu mbili New Africa na huko Moshi pale YMCA ama Moshi Hotel.
Mwaka 1982 kweli madisco yalifunika kabisa miziki ya magita!.Msasani, Rungwe, Slversand,Italian club (clouds), Keys Hotel, Motel Agip, New Africa, Twiga Hotel, Dar Institute na sehemu nyingine kibao ambazo siwezi kuzimaliza.

Seydou alikuwepo Mbowe hadi 1985 wakati Freeman alipoamua kufungua RSVP kuwaondoa Space 1900 ambao walihamishia makazi yao sewhemu mbili New Africa Hotel na Pale Maggot.

Toka wakati huo Seydou hakuwa na mahala maalum kwani Space 1900 ilivunjika kutokana na matatizo ya ndani. Hata hivyo jina Space 1900 liliendelea kutumika na ndio vijana wengine akina Super Deo,Young Millionea wakaibuka.

Hivi sasa DJ Seydou ni mshauri wa muziki wa sehemu mbalimbali ikiwa ni pamoja na Club Ambience ya Sinza na Sanaa Pub. Hazina ya muziki wa zamani na wa sasa aliyonayo haina mfano.

Uliwahi kuhudhuria disco la DJ Seydou?
 

Attachments

  • 1408736361569.jpg
    1408736361569.jpg
    46.7 KB · Views: 180
Dj Seydou na Jerry Kotto ndio Madj wa pale Hisaje maeneo ya Boko.

Kuna kipindi alichoka sana akawa anapiga kwenye vijibaa vya mtaani hadi alipoibukia Fairway pale tegeta na kuanza tena kuwika....sasa hivi ukitaka kucheza disko lake yeye na Jerry Kotto wapo Hisaje na wanafunika ile mbaya .......
Mimi nikiwa mdogo namkumbuka sana Dj Muddy wa Arusha hasa na disko lake la pale Police officers Mess.......
 
Back
Top Bottom