OC-CID
JF-Expert Member
- Jul 13, 2023
- 200
- 463
Leo nimemkumbuka winga hatari wa zamani wa timu ya taifa ya wanawake ya Tanzania “Twiga stars” Esta Chabruma.
Huyu dada alikuwa na uwezo mkubwa sana hasa akitokea pembeni, angeweza kufunga magoli au kutoa assist maridhawa (assist) kwa wenzake kiasi cha kufananishwa uchezaji wake na Winga wa zamani wa Yanga, Edibily Jonas Lunyamila.
Ni miongoni mwa akina dada wa mwanzo kucheza soka la ushindani Tanzania na kufungua njia kwa wadada wengine kujitokeza kucheza mchezo huo unaoonekana kama mchezo wa kiume zaidi.
Siku hizi naambiwa ni kocha mkuu wa JKT Queens ambayo ni timu tishio kwenye Ligi Kuu ya Wanawake nchini.
Nimeamua nimpe maua yake angali akiwa hai💐💐