1. Alinilipia deni la vitabu viwili vilivyoibiwa nikiwa kidato cha pili mwezi wa 11 bila ya mimi kumfahamu. Nikiwa kidato cha tatu niliibiwa begi na vitabu ndani yake, wakati nimefikishwa staff natishiwa adhabu, alikuja na vitabu vipya viwili na kumkabidhi yule mwalimu. Mwalimu akamuuliza, "Tena! Unamlipia deni kwa mara nyingine! Kwani wewe na huyu ni ndugu?". Kesi ikaishia hapo. Wiki moja baadae alinifungukia, japo alikuwa anatetemeka na kutokwa jasho jingi huku akimung'unya maneno[emoji23][emoji23]
2. Kuna kipindi nilichelewa kufika shuleni kwenye zamu ya yule mwalimu aliyekosana na mkewe[emoji23][emoji23] Akanipatia adhabu ya kufanya usafi ofisi ya taaluma baada ya muda wa vipindi. Huyu kaka alinambia nikapumzike mahali, yeye atafanya peke yake. Na kweli alisafisha vyema mpaka walimu wakanisifia kesho yake
3. Kuna mwalimu mmoja hivi wa kiume alikuwa ni zoazoa, anatumia nafasi yake kulazimisha ngono. Baada ya kuona napingana nae alianza kunipatia adhabu za hapa na pale na vipigo. Kuna siku kanikata kibao cha nguvu darasani bila kosa, huyo kaka kainuka pale na kumpatia kipigo maskini[emoji23] mpaka mdomo wa yule mwalimu mshnz ukapasuka vipande viwili kama pazia la hekalu[emoji23] Akafukuzwa shule kwa kunitetea mimi
Nimeyakumbuka haya yote baada ya kukutana na profile yenye picha yake kwa mtandao wa facebook
We unamkumbuka yupi kwa yapi?