Unamkumbuka Murtaza Lakha?!

Sajenti

JF-Expert Member
Joined
Apr 24, 2008
Posts
3,651
Reaction score
413
Kuna advocate mmoja kwa jina la Multaza Lakha kwa wale waliokuwa wakifuatilia ile kesi ya uhaini miaka ya 80. Huyu bwana kwa kumbukumbu zangu ni miongoni mwa mawakili waliokuwa mahiri sana nyakati zile. Kwenye ile kesi ya uhaini iliyowahusisha akina Zacharia Hans Pope, Mr & Mrs Banyikwa, Capt. Eugene Maganga na wengine.

Multaza Lakha aliwahi kumhoji aliyekuwa mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dodoma wakati huo Mzee Ndejembi na mtoto wake kama mashahidi wa upande wa mashtaka. Mpaka leo bado nakumbuka jambo moja ambalo Lakha alimwambia mtoto wa Ndejembi alipokuwa akitoa ushahidi wake..... hapo ni baada ya Ndejembi kuchemsha katika kujibu maswali ya Lakha..

Nanukuuu " yaani wewe na baba yako mmetoka Dodoma kuja hapa kutoa ushahidi wa uongo??"... Ni kesi ya miaka mingi sana lakini nilikuwa nikiifatilia ingawa bado nilikuwa mwanafunzi. Kuna yeyote anayejua aliko huyu Murtaza Lakha???:A S 39::A S 39:
 
Advocate Lakha alienda Uingereza kwenye miaka ya katikati ya 1980s... ni kama alikimbia nchi kiaina inavyosemekana.
 
Murtaza Lakha, nakumbuka kusoma exchanges za mahakamani za kesi ya uhaini katika Mfanyakazi kila Jumamosi. Enzi hizo za kina Jame Nhende, kabla hata ya Stan Katabalo (RIP) na Loliondogate.

Eighties babies hawawezi kuelewa, y'all make me feel old already.

Hivi Mfanyakazi bado lipo?
 
Ya, Alikuwa ni advocate maarufu sana na machachari katika enzi zake, baada ya ile kesi ya uhaini hakusikika tena, sijui nini kilimpata
 
...Ni MuRtaza Lakha. Hivvi wako wapi James Nhende na lile 'trupu' lao la Mfanyakazi ya wakati ule ambao kuna wakati ilikuwa inaongoza kwa mauzo katika magazeti yote nchini?
 
Pia niliwahi kusoma series ya story za Capt. Eugene Maganga kwenye gazeti la Rai mwaka 2007. Kwa kweli jamaa alivyokuwa anaelezea ile habari na anataja maeneo mengi ambayo harakati zao zilikuwa zikifanyika nadhani kama angeandika kitabu nina imani kingepata soko sana...
 
...Ni MuRtaza Lakha. Hivvi wako wapi James Nhende na lile 'trupu' lao la Mfanyakazi ya wakati ule ambao kuna wakati ilikuwa inaongoza kwa mauzo katika magazeti yote nchini?
..James Nhende yuko Mwanza ameanzisha magazeti kama sio gazeti lake moja linaitwa kasi mpya lingine nimesahau jina.
 
..James Nhende yuko Mwanza ameanzisha magazeti kama sio gazeti lake moja linaitwa kasi mpya lingine nimesahau jina.

...Asante Mkuu. Kulikuwa na wale waandishi waliojipa jina la sijui 'Maluteni wa burudani' Charles Charles, Rashid Zahor na Hemed Kimwaga waliishia wapi??
 
Huyu charles Charles amekuwa mwandishi mamluki; unamkodisha anakuandika kunyoosha mambo a' la wakina Ra na EL!1
 
Kwakweli Mfanyakazi la enzi zile ndo angalau lilikuwa wazi maana enzi zile UHURU,MZALENDO na DAILY/SUNDAY NOISE tuu... Mpiga picha Senga sijui yuu wapi... Nadhani Hemed Kimwaga ameshatangulia mbele ya haki... Mwaweza nisahihisha!
 
Ya, Alikuwa ni advocate maarufu sana na machachari katika enzi zake, baada ya ile kesi ya uhaini hakusikika tena, sijui nini kilimpata
Namkumbuka pia wakili muccadam. Kimsingi kesi ile ilitikisa njiiiii hiii mpaka ikaondolewa mahakamani njii ilikuwa na wanasheria makini.
 
Kwakweli Mfanyakazi la enzi zile ndo angalau lilikuwa wazi maana enzi zile UHURU,MZALENDO na DAILY/SUNDAY NOISE tuu... Mpiga picha Senga sijui yuu wapi... Nadhani Hemed Kimwaga ameshatangulia mbele ya haki... Mwaweza nisahihisha!

...Mkuu, sina hakika sana na hili. nadhani Kimwaga bado yupo hai ingawa sina hakika kwa asilimia mia%. tafadhali hebu cheki tena source zako...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…