Unamkumbuka mwalimu wako wa darasa kuanzia la kwanza mpaka ulipomaliza shule?

Unamkumbuka mwalimu wako wa darasa kuanzia la kwanza mpaka ulipomaliza shule?

Joined
Aug 18, 2019
Posts
80
Reaction score
177
Eti je, unamkumbuka mwalimu wako wa darasa kuanzia la kwanza mpaka ulipo maliza shule? Je,unakumbuka wimbo wa shule ya msingi uliposomea?

Je, ni tukio gani huji kulisahau kamwe katika maisha yako ulilofanya au kukutokea ukiwa shuleni? Je,unakumbuka jina kamili la mwalimu mkuu wa shule ya msingi uliosomea?

SOMA >a, e, i, o, u hahahaaa basi hapo nimekukumbusha mbali lakini kumbuka maisha hayo kwako hayatajirudia tena kamwe mpaka utakapokufa na hata ukifa bado hayata jirudia tena mpaka Mungu mwenyewe apange vinginevyo basi ndiyo imetoka.

~NIWATAKIE USIKU MWEMA.
 
Nilichapwa na walimu ofisi nzima kisa nilimtukana afisa elimu alikua amekamata mpira wetu.
 
Wangu ni hawa primary.... nimejaribwu kuwataja taja...

Ms. Peterson
Mr. Conchur
Ms. Kieran
Ms. Taylor
Mr. White
Mr. Watson
Ms. King
Ms. Ward
Ms. P. Relish
Ms. W. Relish
Mr. Jones
Mr. Patel
 
Walionifundisha Ubagwe primary ninaowakumbuka

Mwalimu Bashiru huyu Mhaya alipenda sana sigara na kuvaa koti hata kama kuna jua kali, Jamaa alikuwa mkali balaa.

Mwalimu Marando huyu alichapa viboko visivyo na idadi.

Robert Siwale; Huyu jamaa alikuwa smart sana mtanashati ndio mwalimu wa kwanza kumiliki simu.
Alikuwa anajiona Ronaldo na mpenda totoz sana.

Mgunda; Huyu mwalimu mfupi halafu msela sana.

Furahisha : Huyu msela fulani hivi ila kwa sasa kawa mnywa viroba.

Saida huyu darasa la pili; Huyu Muha nilikuwa namwelewa sana..
 
Back
Top Bottom